Mfuko
 wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) umekamilisha awamu ya kwanza 
ya ujenzi wa nyumba 641 katika mikoa mitano ambazo zilianza kuuzwa tangu
 Novemba mwaka 2012. Mradi huo unalenga kutatua tatizo la makazi kwa 
wanachama wake na jamii kwa ujumla.
Mikoa
 iliyojengwa nyumba hizo na idadi ya nyumba katika mabano ni Dar es 
salaam – Buyuni (491), Morogoro – Lukobe (25), Shinyanga – Ibadakuli 
(50), Tabora – Usule (25) na Mkoa wa Mtwara – Mang’amba (50).
Aidha
 kwa Mujibu wa maelezo ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bwana Adam 
Mayingu amewaambia wanandishi wa habari na viongozi mbalimbali 
waliotembelea eneo la mradi huo Mkoa wa Dar es Salaam kuwa Shirika lake 
limejenga nyumba za aina nne ambazo ni za nyumba viwili, Vyumba vitatu, 
Nyumba za vyumba vitatu kimoja ikiwa ni Master na Nyumba ya vymba vine 
kimoja kikiwa ni Master.
Gharama
 ya ununuzi wa nyumba hizo ambazo zinauzwa kwa wanachama wa Mfuko huo ni
 kati ya Shilingi Milioni 64 hadi milioni 94 gharama zikijumlishwa na 
Kodi ya ongezejo la Thamani.
Kaimu
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) Adam 
Mayingu (katikati) akiwaonesha maofisa wa Jeshi la Polisi moja ya nyumba
 491 zilizopo katika mradi wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu ambazo 
zitkopeshwa kwa wanachgama wa mfuko huo. Nyumba hizo zipo katika eneo la
 Kigezi Kata ya Majohe wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam. 
Kaimu
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) Adam 
Mayingu (kushoto) akifafanua jambo wakati wa ziara hiyo ya kuakagua makazi hayo. Kulia ni  Naibu 
Meya wa Manispaa ya Ilala, Hery Mohamed Kessy Nyumba hizo zipo katika 
eneo la Kigezi Kata ya Majohe wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam.
 
 Ziara ikiendelea katika nyumba hizo zipatazo 491 





