KAMPUNI
 ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Kilimanjaro Premium Lager 
imekabidhi jezi kwa timu za Simba na Yanga kwa ajili ya mechi ya Nani 
Mtani Jembe itakayochezwa Jumamosi kuanzia saa kumi kamili jioni kwenye 
Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kampeni ya Nani Mtani Jembe iliyozinduliwa Oktoba 6 mwaka huu itamalizika Jumamosi kwa klabu za Simba na Yanga kuchuana vikali pamoja na kuwania Sh milioni 100 zilizotengwa na Kilimanjaro Premium Lager ambao ni wadhamini wakuu wa timu hizo.
George
 Kavishe akiwakabidhi Makamu Mwenyekiti wa Simba, Joseph Itangare 
na Msemaji wa Yanga, Baraka Kizuguto jezi maalum zitakazotumika kwenye 
mechi ya Nani Mtani Jembe Jumamosi tarehe 21 Desemba.  
Akizungumza
 na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Meneja wa Kilimanjaro 
Premium Lager George Kavishe alisema wanakabidhi vifaa hivyo vyenye 
thamani ya Sh milioni 6.8 kwa ajili ya kuzipa mwonekano mpya timu hizo 
katika mechi hiyo.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Simba Joseph Itang’are ‘Mzee Kinesi’ aliwashukuru wadhamini hao Bia ya Kilimanjaro kwa vifaa hivyo huku akitamba timu yake kuibuka na ushindi.
Naye Ofisa Habari wa Yanga Baraka Kizuguto aliwashukuru wadhamini hao kwa kuwafanyia mambo mazuri na kuahidi kuendeleza mambo mazuri kwao na wataibuka na ushindi katika mechi hiyo.
