Askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), wakiwa wameinamia kwa 
huzuni  jeneza lenye mwili wa  askari mwenzao, marehemu Luteni Rajab 
Mlima wakati wa maziko yaliyofanyika jana katika makaburi ya Kisutu, Dar
 es Salaam jioni hii. Mlima ambaye alikuwa katika Jeshi la Umoja wa 
Mataifa la Kulinda Amani DRC Congo aliuawa akiwa kazini katika Mlima 
Gavana eneo la Goma.
Waombolezaji wakijiandaa kufanya maziko
Waombolezaji wakifanya maziko
Askari wa JWTZ wakitoa heshima wakati wa maziko
Meja Leonidas Luangisa akisoma wasifu wa marehemu Luteni Mlima.
Mseamaji Mkuu wa Familia ya Mlima, Balozi Alhaji Saleh Tambwe akisoma
 salamu za familia na kuwashukuru watu wote walioshiriki kwenye mazishi 
hayo.