Msafara  wa rais Jakaya  Kikwete ukiwa 
 umesimama kwa muda eneo la  msitu wa  taifa  wa Sao Hill Mufindi  
katika barabara kuu ya Iringa- Mbeya  kufuatia  moto mkubwa kuwaka 
katika msitu huo.
 Askari polisi akimamisha  msafara  wa 
rais Kikwete kutokana na moto  mkubwa  kutanda  eneo hilo la Changalawe 
katika  msitu wa Taifa  wa Sao Hill umbali wa mita  mbili kuelekea  
barabara  ya Ikulu ndogo mjini Mafinga 
 Askari  wa FFU  wakishuka katika gari 
lao kwenda  kuangalia  usalama  wa rais Kikwete na  kulia gari la kwanza
 ni naibu waziri wa ujenzi gari la pili na la tatu ni magari ya Ikulu 
yakiwa  yamesimama 
 hapa  askari  wakishuka  kuingia katika
 moshi mzito  kuangalia  usalama  wa rais katika eneo hilo ambalo moshi 
mzito  ulitanda barabarani
 Msafara  ukipita  eneo hilo salama huku kulia ni askari wa JKT mafinga wakizima moto  huo 
Yakiwa ni masaa takribani mawili  kupita  kutoka Rais Jakaya  Kikwete kufanya 
 kikao chake  cha majumuisho   ya ziara  yake   na  viongozi wa mkoa wa 
Njombe na  kuwataka  kuchukua hatua  katika kuthibiti moto  ili  
kuepusha ukame ,moto  mkubwa umezuka katika msitu wa Taifa  wa Sao Hill 
Mufindi na kupelekea  msafara  wa  Rais kusimama kwa  muda  kiusalama 
kutoka na moshi mzito  uliotanda  barabara  kuu ya Iringa Mbeya .
Moto 
 ulio ulioanza  kuwaka  mida ya saa nane  mchana    ulizuia kwa  muda  
kama dakika tatu hivi msafara  wa Rais Kikwete  kufimama katika eneo la 
Changalawe mjini  Mafinga umbali  wa mita 2  kufika  njiapanda  ya   
kuingia ofisi ya mkuu  wa wilaya ya  Mufindi na Ikulu ndogo  ya  wilaya 
ya Mufindi.
Kutokana
 na tukio hilo la moto msafara  wa rais  Kikwete  ulisimama na baada ya 
maofisa  usalama  kushuka na kutazama usalama  zaidi wa msafara  huo 
ndipo  walioruhusu msafara  huo  kuendelea .
Hata 
 hivyo  jitihada  kubwa  zilionekana kufanywa na  kikosi  cha askari  
wa  JKT Mafinga  pamoja na  wananchi ambao  walikuwa  wakizima  moto  
huo .
Huku  
 vyombo  vya  usafiri  yakiwemo mabasi ya abiria yanayosafiri  kutoka Dar
 es Salaam kuwenda  mikoa ya  kusini na nchi  za kusini mwa Tanzania 
yakikwama  kuendelea na  safari  kutoka na moto  huo kushikakasi na  
moshi  mzito  kutanda  barabara 
Mkuu 
 wa  mkoa  wa  Iringa Dr  Christine Ishengoma  alisema kuwa  uongozi  
wa  mkoa  tayari  umeagiza  mkuu wa wilaya ya Mufindi kuwasaka   
waliohusika na  uchomaji  moto huo ili  kuchukulia  hatua  kali.
Mkuu 
 huyo  wa  mkoa alisema  kuwa mkoa  wa Iringa umekuwa  ukichukua hatua  
kali  kwa wale wote wanaoanzisha  moto  kichaa kama  huo hivyo  kupitia 
 ofisi ya mkuu wa wilaya ya Mufindi wahusika  watasakwa  popote  walipo .
Mbali
 na  hilo mkuu  huyo amelipongeza  jeshi la JTK Mafinga kwa  kuchukua 
hatua  za haraka katika kukabiliana na moto  huo huku akisema madhara  
zaidi  yatokanayo na moto  huo yatatolewa baada ya  moto  huo 
kuthibitiwa Chanzo: Francis Godwin-Iringa