Marehemu Zakaria Gindu baada ya kujilipua na moto.
Mkazi
 wa kitongoji cha Kijiweni kilichopo kijiji cha Chifunfu kata ya 
Chifunfu wilaynia Sengerema mkoa Mwanza, amefariki dunia baada 
yakujilipua kwa moto kisha kuungua vibaya na kufariki dunia akiwa ndani 
ya nyumba yake.
Akithibitisha
 kutokea kwa tukio hilo Mwenyekiti wa kitongoji hicho Bw. Juma Mashauri,
 amemtaja aliyekumbwa na mauti hayo kuwa ni Bw. Zakaria Ngindu (36) 
mzaliwa wa kijiji cha Mwamanyiri wilaya ya Busega  Mkoa wa Simiyu.
Bw. 
Mashauri amesema kuwa tukio hilo lilitokea mnamo Septemba 27 mwaka huu 
majira ya saa10 jioni na chanzo cha tukio hilo inaelezwa kuwa ni 
kutokana na ugomvi uliokuwa ukiendelea ndani ya nyumba yake na mke wake 
aliyetajwa kwa jina la Veronica Lumanicha mzaliwa wa kitongoji cha Ngoma 
‘B’ Kilichopo kijiji cha Nyamatongo Kata ya Nyamatongo wilayani 
Sengerema, baada ya kumkuta akiwa na namba za simu ya mkononi ambazo 
hazieleweki kuwa ni za nani.
Kwa 
mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo walisema wanandoa hao walikuwa na 
ugomvi wa mara kwa mara wakituhumiana kutokuaminiana katika ndoa yao 
iliyokuwa imegubikwa na vitimbwi vingi vilivyosababisha mmoja  wa 
wanandoa hao kushikwa na hasira na kunywa pombe kisha kuchukuwa maamuzi 
ya kujiua ili kuondokana na kero hiyo.
Kutokana
 na tukio hilo kwa upande wake  Katibu wa umoja wa vijana wa chama cha 
mapinduzi (CCM) wilaya Sengerema Bw.Benedictor Bujiku aliyekuwa 
ameambatana na waandishi wa habari kushuhudia tukio hilo amewaomba 
vijana kupenda kujishugulisha na shuguli na kuacha suala la ulevi 
unaosababisha kuchukua maamuzi ya kujiua wakati Taifa bado linawategemea .
Naye
 diwani wa kata hiyo Robert Madaha amesikitishwa kwa kutokea
 kwa tukio hilo na amewataka wananchi kuacha unywaji wa pombe ambao 
hauna faida yoyote kwa ujenzi wa Taifa.
