WAZEE wa Yanga waliokasirika na 
'kuipiga laana' timu baada ya kutofautiana na aliyekuwa Mwenyekiti wa 
klabu wakati huo, Wakili Lloyd Baharagu Nchunga ikapigwa 5-0 na Simba SC
 mwaka juzi, wameingia katika mgogoro mwingine na uongozi wa sasa chini 
ya Mwenyekiti, Alhaj Yussuf Mehboob Manji.
        
Wazee hao chini ya kinara wao, Ibrahim
 Ally Akilimali wanaingia katika mtafaruku na uongozi wa Manji, kiasi 
cha mwezi mmoja na ushei kabla ya mchezo mwingine dhidi ya watani wa 
jadi, Simba SC Oktoba 20, mwaka huu, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
 
Hatumtaki
 huyo Mkenya; Kutoka kulia Mzee Bilal Chakupewa, Ibrahim Akilimali na 
Hashim Muhika. Wazee hao wamesema hawatambui ajira ya Mkenya.
 
Katika Mkutano wao na Waandishi wa 
Habari leo makao makuu ya klabu, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani,
 Dar es Salaam, Wazee hao wanapinga mambo mawili yaliyofanywa na uongozi
 wa Manji; kuleta Mhasibu mwenye asili ya Kiasia na kuajiri Katibu mpya 
kutoka Kenya.
 
Katibu Mkuu mpya 
wa Yanga SC, Patrick Naggi yupo tayari nchini kuanza kazi akirithi 
mikoba ya Lawrence Mwalusako aliyemaliza Mkataba wake.
 
Akizungumza
 na Waandishi wa jhabari klabu leo, Mwenyekiti wa Wazee hao, Ibrahim 
Akilimali amesema kiongozi yeyote ambaye anapaswa kuiongoza Yanga, 
lazima awe mwanachama wa klabu hiyo, hivyo walivyofanya uongozi ni 
kinyume kabisa na Katiba inavyotaka.
 
"Mpaka
 sasa sisi hatumtambui, kwani hatuna vielelezo vyake vya kuwa mwanachama
 wa klabu hii, endapo atatuletea vielelezo hivyo sisi tutamtambua na 
kumpa ushirikiano.
"Kazi za Wanayanga zitafanywa na wanachama wetu pekee na si wa nje ya klabu yetu, hatutakubali hata chembe kuona katiba yetu ikikanyagwa na viongozi wetu, tutasimama kidete mpaka mwisho kuona jambo hili halifanikiwi," alisema Akilimali
 
Alisema wao 
wakiwa kama wanachama wa Yanga hawatambui ajira ya raia huyo wa Kenya na
 anatakiwa kuondoka ndani ya saa 24 klabuni hapo.
Akilimali alisema hawataki kumwona katika klabu hiyo, kwani Yanga ina wasomi wengi ambao wanaweza kuifanya kazi hiyo.
 
Akilimali alisema hawataki kumwona katika klabu hiyo, kwani Yanga ina wasomi wengi ambao wanaweza kuifanya kazi hiyo.
Alimfananisha
 Mkenya huyo ni mtu aliyeingia kwa njia za panya katika klabu hiyo, kwa 
kuwa hawana mwanachama wa aina yake kwenye leja ya wanachama wa Yanga.
Alisema wamekuwa na kawaida ya kupewa taarifa na Mwenyekiti wa Klabu hiyo, Manji kama kunakuwa na jambo lolote ambalo wamepanga kulifanya kwa maslahi ya Yanga, lakini hawakuambiwa kuhusu ajira ya Mkenya huyo.
 
"Huyu mtu tunamwona ni 'kanjanja' aondoke haraka sana, sisi wana Yanga hatumuitaji kabisa," alisema Akilimali.
 
Wakati
 huo huo, mwanachama wa klabu hiyo, Said Motisha alisema Yanga 
itagawanyika kwa hilo, kwani hawatakubali wazawa kunyimwa ajira wakati 
wanasifa ya kufanya kazi.