Pages

Tuesday, September 17, 2013

CHADEMA KUMSHITAKI BALOZI WA CHINA UMOJA WA MATAIFA

CHADEMA iimesema itamshitaki Balozi wa China nchini, Lu Younqing Umoja wa Mataifa (UN) kwa kukiuka Mkataba wa Vienna (Vienna Convention) wa mwaka 1964 ambao unaeleza uhusiano wa kibalozi kati ya nchi na nchi.

Aidha, kimesema kitaiandikia barua Serikali ya China ili kutaka ufafanuzi kama imemtuma Balozi wake kufanya kazi ya uenezi siasa kwenye vyama baada ya Balozi huyo kuhudhuria mkutano wa hadhara wa CCM Septemba tisa mwaka huu kwenye mkutano wa chama hicho uliofanyika Wilaya ya Kishapu Shinyanga, ambapo Katibu Mkuu wake, Abdulrahman Kinana alimtambushisha Balozi huyo huku akiwa amevaa sare za chama hicho.