Sakata
 la klabu ya Yanga kugomea kukubaliana na mkataba wa kati ya kamati ya 
Ligi na Azam Media wa kuipa haki za matangazo ya televisheni ya mechi za
 ligi kuu kituo cha Azam TV limechukua sura mpya baada ya Raisi wa 
shirikisho la soka la nchini TFF Leogdar Tenga  kuingilia kati.
Kwa
 mujibu wa taarifa rasmi mtandao huu ulizozipata ni kwamba Tenga 
amewaandikia barua Yanga akiwaambia kwamba amepata malalamiko yao dhidi 
ya mkataba wa urushwaji wa matangazo ya mechi za ligi kupitia Azam TV.
Pia
 Tenga amewaambia Yanga kwamba ameiomba kamati ya ligi kumpatia maelezo 
namna mchakato mzima wa ugawaji wa tenda hiyo ulivyofanywa mpaka kufikia
 maamuzi ya kuingia makubaliano na Azam TV.
Tenga
 amewaomba Yanga kuwa wavumilivu ili kushughulikia malalamiko yao 
kuhakikisha muafaka unafikiwa kwa ajili ya manufaa ya soka la Tanzania.
SOURSE: SHAFFIH DAUDA 
