| Mhe. Membe akimkabidhi shada la maua Dkt. Tax kwa niaba ya Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje mara baada ya kuwasili Wizarani hapo. | 
| Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John Haule nae akimkarisha Dkt. Tax kwa furaha Wizarani. | 
| Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Irene Kasyanju akimpongeza kwa shada la maua Dkt. Tax mara nbaada ya kuwasili Wizarani. | 
| Dkt. Tax akipongezwa na kukaribishwa Wizarani na Naibu Katibu Mkuu, Balozi Rajabu Gamaha. | 
| Balozi mpya wa Tanzania nchini Ethiopia, Mhe. Naimi Aziz, nae pia aliungana na Wafanyakazi wa Wizara kumpongeza dkt. Tax. Anayeshuhudia pembeni ni Bw. Ali Mwadini, Katibu wa Naibu Waziri. | 
| Dkt. Tax akipongezwa na Bw. Omar Mjenga, Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Asia na Australasia huku Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango, Bw. James Lugaganya (kushoto) akishuhudia. | 
| Balozi Bertha Semu-Somi, Mkurugenzi wa Diaspora akimlaki kwa shangwe Dkt. Tax wakati wa mapokezi. | 
| Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati, Balozi Simba Yahya nae akitoa pongezi zake za dhati kwa Dkt. Tax | 
| Maafisa mbalimbali wa Wizara nao pia walikuwa mstari wa mbele kumpongeza Dkt. Tax. | 
| Dkt. Tax akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya mapokezi makubwa aliyoyapata kutoka kwa Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, huku Mhe. Membe akishuhudia. | 
| Mhe. Membe akifurahia jambo na Makatibu Wakuu wakati Dkt. Tax akisaini Kitabu cha Wageni.Picha na Reginald Philip. |