Kiongozi mmoja wa usalama nchini Misri ametangaza kuwa, wanachama 38
 wa Harakati ya Ikhwanul Muslimin wameuawa, katika tukio la mapigano 
kati ya askari polisi na watu waliokuwa na silaha, waliotaka kuwatorosha
 watu hao kutoka gerezani. 
Habari zinasema kuwa, mapigano hayo yalitokea
 karibu na jela ya Abu Zaabal katika mkoa wa al-Qalyubiyah. Aidha 
wafungwa hao walikuwa wamemteka polisi mmoja katika mapambano hayo.
 Wizara ya Mambo ya Ndani nchini Misri imetangaza kuwa, polisi 
walifanikiwa kumuokoa polisi huyo ambaye alikuwa amejeruhiwa vibaya. 
Jana wafuasi wa Ikhwanul Muslimin walisitisha maandamano mjini Cairo kwa
 kile walichosema kuwa ni kuepusha umwagikaji damu zaidi dhidi yao.  
Ripoti iliyotolewa na harakati hiyo, ilisema kuwa, Ikhwan wameamua 
kusitisha maandamano yao, kutokana na kuwepo hali tete nchini humo. 
Kabla ya hapo, ilikuwa imepangwa kufanyika maandamano ya nchi nzima, kwa
 ajili ya kutaka kurejeshwa Muhammad Mursi, Rais halali wa Misri 
aliyepinduliwa na jeshi la nchi hiyo.
