JESHI
 LA wananchi wa Tanzania (JWTZ), limetoa ufafanuzi kwa kusema kuwa 
askari wake aliyetoroka jeshini Luteni Kanali Coelestine C. Seromba kwa 
kusema kuwa ni mzaliwa wa Kagera na siyo Rwanda.
Jeshi hilo limevitaka vyombo vya habari kuacha kuripoti taarifa potofu za afisa huyo ambaye alikuwa akikabliwa na tuhuma za makosa ya kijeshi na baadaye akatoweka wakati mchakato wa kumfungulia mashitaka ukiendelea.
Msemaji wa Jeshi hilo Meja Erick Komba Tamba akizungumza na wanahabari Dar es Salaam siku ya Jumamosi, alisema Seromba alitoroka Desemba 17 mwaka jana baada ya kuona kosa lililokuwa linamkabili linaweza kumtia hatiani, hatua ambayo amesema haina madhara kwa jeshi hilo. Kwa kuwa Lut. Kan. Seromba alitambua kuwa ametenda kosa na kuamua kutoroka, hatua ambayo ni kinyume cha sheria za JWTZ, ataendelea kutafutwa na akipatikana, atafunguliwa mashitaka kwa kosa la kutoroka JWTZ.

---
Blog moja inasema
 kutokana na serikali kupenda kuajiri vyeti badala ya watu, kuna kundi 
kubwa la askari wa majeshi ya Tanzania ambao siyo raia wa nchi hii na 
inasisitiza kuwa imewahi kuripoti uwepo wa raia wa Rwanda na Burundi 
katika majeshi ya Tanzania