
.
Ni ngumu kumuona mwanaume akitokwa machozi kama hivi…. hii 
imetokana na mke wake kumpiga makofi hadharani kwenye mji wa Meru nchini
 Kenya ambapo Mwanamke huyo alikua anadai jamaa kamkana, japo 
anasisitiza kwamba ni mume wake na ndio baba wa watoto mapacha akiwemo 
mmoja alienae mgongoni, Mwanaume alikataa kabisa na kusema hata watoto 
sio wake.
Taarifa ambayo imerushwa na KTN Kenya, ni kwamba alichotaka 
Mwanamke ni Mwanaume huyo akubali tu kwamba ni mume wake na pia ndio 
baba watoto wa mapacha hao… lakini Mwanaume aliapa kabisa kwamba hausiki
 kwenye upande wowote, hicho ndio kilichompa hasira Mwanamke na kuanza 
kumpiga na baadae pia kusaidiwa kupiga na Mwanamke aliekua nae.
Kenya imekua kwenye mfululizo wa kesi za Wanawake kupiga 
waume zao nyumbani na hadharani pale wanapokosana ambapo February 2012 
Umoja wa Wanaume Kenya ulitangaza kususia kula majumbani kwa wiki moja 
na kununua chakula hotelini mpaka Serikali itakapoingilia usawa wa 
Wanaume na kuhakikisha tabia ya Wanawake kupiga Waume zao inamalizwa.