| Mkutano
 mkuu wa klabu ya Simba umefanyika leo kwenye Bwalo la Polisi, Osteybay Jijini Dar es Salaam. Mkutano huo ulihudhuriwa na 
wanachama wapatao mia saba ulifanyika kwa saa moja kuanzia saa nne mpaka saa tano kamili asubuhi. Mkutano huo ulizungumzia mambo mengi 
ikiwemo Taarifa ya matumizi ya fedha za klabu, Suala la ujenzi wa uwanja
 wa Simba pamoja na kuzinduliwa kwa mkakati mpya wa maendeleo ya Simba.  |