Bakili
 Makele (kulia) akiongea na waandishi wa habari kwa niaba ya viongozi wa
 matawi, Moses Katabaro(katikati) na Lawrence Mwalusako (kushoto) 
Uongozi
 wa matawi wa klabu ya Yanga (wenyeviti na makatibu) leo umefanya kikao 
katika makao makuu ya klabu mtaa wa twiga/jangwani kisha kutoa tamko lao
 kwa waandishi wa habari kuhusiana na tamko la uongozi (kamati ya 
utendaji) kutokubali kuonyeshwa kwa michezo yake kwenye luninga.
Awali klabu ya Yanga juzi kupitia kamati ya utendaji ilifanya mkutano
 na waandishi wa habari juu ya mustakabali wa klabu kuhusiana na 
kutoridhishwa na kamati ya muda ya Ligi (TPL) kuingia makubaliano ya 
kurushwa matangazo ya televsheni kwenye michezo yake.
Akiongea na 
waandishi wa habari leo katibu mkuu wa Yanga Lawrence Mwalusako alisema 
baada ya kukaa na viongozi wa matawi ya klabu ya Yanga jijni Dar es 
salaam kwa pamoja wamekubali na kuunga mkono hoja zilizowasilisha na 
viongozi juu ya haki ya matangazo.
Mmoja wa viongozi wa matawi 
Bakili Makele akiongea kwa niaba ya viongozi wa matawi, alisema TFF 
inaamua kukandamiza soka la Tanzania kwa kuviamulia maamuzi yake juu ya 
kuonyeshwa kwa michezo ya timu kwenye luninga.
Makele amesema 
taratibu za kuipa kampuni ya Azam TV tenda ya kuonyesha michezo ya Ligi 
Kuu haikua na usawa, kampuni hiyo bado haijaanza hata matangazo, 
haijulikani ofisi zake zilipo, uwezo wa kurusha matangazo haujulikani 
kwa watanzania lakini bado wamepewa nafasi hyo.
Kikubwa tunamuomba
 rais wa TFF Leodgar Tenga kulitazama suala hili kwa umakini, kwani 
mtazamo wetu viongozi wa kamati ya Ligi wametazama maslahi yao binafsi 
bila kuzingatia uwezo wa timu na maliasili watu (wapenzi,washabiki).
Huwezi
 kuipa mgawo sawa timu ya Yanga na timu nyingine ambazo katika mechi zao
 binafsi wanatapata washabiki 50 kwenye mchezo, wakati Yanga imeongoza 
kwa mapato katika msimu mzima wa Ligi Kuu ya Vodacom na wastani wa 
washabiki 8,000 kwa kila mchezo.
Mwisho
 Makele amesema wanauamini uongozi uliopo na wapo nao bega kwa bega, 
tunaomba jamii nzima itambue kuwa Yanga inapigania haki zake na hao wote
 wanaobeza msimamo wetu basi wajibu hoja kwa hoja na sio kuongea tu 
pasipo kujibu hoja. 
SOURSE:YANGA
SOURSE:YANGA