Na Shakoor JongoWAKATI Wema Isaac Sepetu akiongeza idadi ya magari kwa kununua mkoko wa maana, zilipendwa wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amemziba mdomo baada ya kununua eneo kubwa ambalo ndani yake kuna nyumba tatu, jirani na anapoishi Miss Tanzania huyo wa mwaka 2006, Ijumaa Wikienda lina maelezo kamili.
Eneo alilonunua Diamond katika Mtaa wa Kaprikoni-Kijitonyama jijini Dar.
Diamond.
Akizungumza na gazeti, hili muda mfupi  baada ya kukamilisha kila 
kitu kuhusiana na ununuzi wa eneo hilo ambalo kwa mujibu wake anatarajia
 kujenga jengo lenye ghorofa nne na nyumba za kawaida tatu, Diamond 
alisema kuwa anajitahidi kuongeza idadi ya mijengo anayomiliki kwa kuwa 
ndicho kitu cha thamani kuliko magari.
Mkoko wa Wema.
 
Wema.
Katika hali iliyotafsiriwa kuwa ni kumtunishia msuli Wema, jamaa 
alitupia maneno: “Mimi siyo kama hao wanaokimbilia kununua magari ya 
kifahari ili mradi waonekane wako juu kifedha.Eneo alilonunua Diamond anayemiliki nyumba zaidi ya tano Dar lipo mtaa wa nne kutoka anapoishi Wema.