Siku
kadhaa baada ya Baraza la Vyama vya soka Afrika Mashariki na Kati -
CECAFA kuidhinisha michuano ya kombe la Kagame kuchezwa mjini Darfur
-Sudan, serikali ya Tanzania imetoa tamko kuhusu timu za Simba na Yanga
kwenda kushiriki michuano hiyo huko Sudan kwenye eneo ambalo limekuwa
likiandamwa na vurugu kwa miaka kadhaa sasa.
Kwa
mujibu wa msemaji wa klabu ya Simba Ezekiel Kamwaga ni kwamba serikali
haidhani ni busara kwa vilabu vya Simba na Yanga kwenda kwenye eneo hilo
kushiriki Kagame Cup kutokana hali mbaya ya usalama iliyopo Darfur.
HIVI NDIVYO ALIVYOANDIKA KAMWAGA KWENYE UKURASA WAKE WA FACEBOOK.