Kwa zaidi ya wiki moja iliyopita habari zilisambaa kwamba 
binti Mtanzania aliekamatwa na dawa za kulevya nchini Misri angenyongwa 
siku za karibuni kutokana na hizo dawa alizokamatwa nazo.
millardayo.com baadae ilimpata balozi wa Tanzania Egypt ambae
 alikanusha taarifa za kunyongwa na akakubali kwamba kweli kuna 
Watanzania wawili wamekamatwa ambao ni huyo msichana na ndugu yake wa 
kiume ambao ni wakazi wa Magomeni Dar es salaam na kwamba wanashikiliwa 
na polisi huku wakisubiri kesi yao.
Leo hii, kitongoni.blogspot.com inakupatia nafasi kuona video ya 
mahojiano ya TV na msichana huyu ambae anadai alikwenda Misri kumtafuta 
binamu yake, begi alilokamatwa nalo ni lake ila alikua hajui kama lina 
dawa za kulevya.