
 Wachezaji wa Taifa Stars wakiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere Jumatatu alfajiri wakitokea Morocco.


-Asema adhabu ya kadi nyekundu haikuwa na ulazima
-Asema wangecheza 11 ushindi ulikuwa wazi
Kocha
 wa Timu bali matokeo ya Taifa (Taifa Stars), Kim Poulsen amesema refa 
wa mechi ya Taifa Stars na Morocco iliyopigwa Marrakech Jumamosi kusaka 
tiketi ya kucheza fainali za Kombe la  Dunia Brazil mwakani aliuwa 
mchezo kwa kutoa kadi nyekundu kwa mchezaji Aggrey Morris.
Akitoa
 maoni ya mchezo huo, Poulsen alisema alisikitishwa na jinsi refa huyo 
alitoa adhabu kali ambayo haiendani na kanuni za FIFA.
Aggrey
 Morris alioneshwa kadi nyekundu baada ya kugongana na Abderazak Hemed 
Allah ambaye aliifungia Morocco bao la kwanza katika dakika ya 37.
“Hakuwa
 na sababu ya kumuonesha Morris kadi nyekundu kwani tayari alishawapa 
Morocco penalti, alisema Poulsen huku akiongeza, “FIFA imeshawaonya 
marefa mara kadhaa dhidi ya kuua mchezo kwa namna hii ya kutoa adhabu 
kali kupita kiasi.”
Poulsen
 alisifu wachezaji wake na kusema licha ya kucheza pungufu walipambana 
uwanjani na kufanikiwa kupata bao kupitia kwa Amri Kyemba. Morocco 
walishinda kwa 2-1.
“Kama
 tungecheza kumi na moja hadi mwisho nina uhakika tungeshinda mechi hii 
lakini refa aliiua mechi na huwezi kufanya hivi katika mechi ngumu kama 
hii,” alisema Poulsen.
Kocha
 huyo alisema kupata goli la ugenini unapochez na timu ngumu kama 
Morocco ni jambo la kujivunia hasa mnapokuwa pungufu uwanjani.
Alisisitiza
 kuwa sasa wanaelekeza nguvu zote katika mechi shidi ya Ivory Coast 
Jumapili ijayo. “Mambo ya Morocco yamekwisha sasa tunafikiria namna ya 
kushinda mechi ya Jumapili.
Tanzania iko katika kundi C inayoongozwa na Ivory Coast yenye pointi 10, Tanzania 6, Morocco 5 na Gambia 1.
Taifa
 Stars imerejea Jumatatu alfajiri kutokea Marrakech Morocco na 
itaendelea na kambi ya wiki moja ili kujiandaa na mechi dhidi ya Ivory 
Coast.
Nahodha
 wa Taifa Stars, Juma Kaseja alisema wachezaji walicheza kwa ari kubwa 
na walifurahishwa na jinsi watanzania walijitokeza kwa wingi.
“Tulipata faraja kubwa sana kuwaona watanzania wengi uwanjani…mambo ya Morocco yameisha sasa tuangalie Ivory Coast,” alisema.
Meneja
 wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe ambaye bia yake 
inadhamini Taifa Stars, alisema wacezaji walijitahidi hasa ikizingatiwa 
walicheza pungufu na hata wakafanikiwa kufunga bao moja.
“Katika
 hali kawaida, wachezaji wengine wangekata tamaa lakini bao hili moja 
linaonesha kuwa wachezaji walikuwa na ari ya kupata ushindi,” alisema Bw
 Kavishe.
Alisema
 wao kama wadhamini wana imani kubwa na Taifa Stars na kwamba wanaamini 
hii ni safari ya mafanikio ambayo ilianza mwaka mmoja uliopita
SOURSE: MO blog