IKIWA ni siku moja tu tangu Naibu Waziri wa Habari  Michezo
 Vijana na Utamaduni Amos Makala kutangaza hadharani kulivalia njuga 
suala la mzozo kati ya Mkurugenzi wa wa Kampuni ya Clouds Media Group 
Ruge Mutahaba  na msanii nyota wa kike wa Bongo Fleva Judith ‘Wambura Lady Jaydee’  Ruge ametoa ya moyoni.
Tanzania
 Daima ambayo ilimpigia simu Ruge na kumuuliza ana lipi la kusema baada 
ya Makala kutamka kwamba atawaita wawili hao na kuzungumza nao sambamba 
na kuleta suluhu.
“Mimi kana nilivyosema katika tamko langu wiki iliyopita kwamba niko tayari tuitwe na watu watusikilize  pande zote mbili  hasa
 mlalamikaji na ukweli uweze kuwa wazi zaidi kwa sababu hadi sasa Lady 
Jaydee amekuwa akisema mambo mengi kiasi kwamba hata nashindwa 
kumuelewa”
Na siyo Waziri Makalla tu pia ikiwezekana hata kama
 kuna watu wengine wanataka kujitokeza ili kutuweka katika kiti moto 
watuulize maswali na kila mmoja wetu aote majibu mbele ya hao watu mimi 
niko radhi kufanya hivyo” anasema Ruge.
Wakati huohuo Ruge ameongeza kwamba  tayari
 ameshafuata taratibu za kisheria ikiwa ni pamoja na kumfungulia 
jalada la malalamiko ya kutukanwa na Lady Jaydee na taarifa hiyo 
amepelekewa  msanii huyo akiitwa katika vyombo vya sheria.
Lakini
 ninaweza kusema jambo hili linaweza kuzungumzika nje ya vyombo vya 
sheria kwani sisi tunaliona ni jambo dogo na la mzaha lakini lina athari
 kubwa katika jamii inayotuzunguka  anasema Ruge.
Mwanzoni mwa mwezi huu Lady Jaydee aliamua kuibuka na kuituhumu Clouds Media Group  kwa
 kutumia mitandao ya kijamii kama facebook, twitter nab log yake kwamba 
wana muhujumu kimuziki , kuzuia matangazo ya mgahawa wake wa Nyumbani 
Lounge   na kipaji chake kwa ujumba tuhuma ambazo Ruge na Clouds wanazikanusha vikali.
Mwandishi
 wa habari hii alijaribu kumtafuta Lady Jaydee azungumzie kuhusu kauli 
ya Waziri kwa kupitia simu ya mumewake Gadner Habash simu iliita bila 
kupokelewa.
