KENYA-- Padri wa kanisa Katoliki amekutwa amekufa baada ya kujiua leo
asubuhi katika eneo la Turkana siku moja baada ya kufikishwa katika
mahakama ya Lodwar kwa madai ya kumlawiti mwanafunzi wa kidato cha tatu.
Mwili
wa John Manzi ulipatikana ukining’inia katika makazi ya mapadri
dayosisi ya Lodwar Jumatano, siku moja baada ya kuachiliwa kwa dhamana
ya KSh100,000 na kaimu hakimu mwandamizi Harrison Barasa.
Afisa
mkuu wa polisi Turkana Kati John Onditi, alisema maiti ya kasisi huyo
ilipatikana ikining’inia nyumbani kwake Jumatano asubuhi.
Upande
wa mashitaka ulikuwa umedai kuwa padri huyo alimshawishi mvulana huyo
mwenye umri wa miaka 18 nyumbani kwake Ijumaa usiku ambapo walipata
vileo kabla ya kutekeleza kitendo hicho mwathiriwa akiwa amelewa.
Mwanafunzi
huyo aliamka asubuhi na kugundua kuwa padri huyo alikuwa amemlawiti
kabla ya kupiga ripoti polisi akiwa ameandamana na mzazi wake.
Marehemu
kisha alijisalimisha mwenyewe kwa kituo cha polisi cha Lodwar baada ya
kudokezewa kuwa mvulana huyo amepiga ripoti polisi.
Kuachiliwa
Tukio
hilo liliibua maswali miongoni mwa waumini wa kanisa hilo na makasisi
wengine waliojazana katika kituo hicho cha polisi wakimtaka padri huyo
awachiliwe.
Daktari aliyemchunguza
mwathiriwa alithibitisha kuwa matokeo yake yanaambatana na madai ya
mvulana huyo ya kulawitiwa. Vile vile, madaktari walisema kuwa mvulana
huyo anapokea ushauri hasa baada ya kutatizwa sana na tukio hilo.