
Jose Mourinho Ametangazwa Kama Kocha 
mpya wa Chelsea chini ya mkataba wa miaka 4 wenye thamani ya Pauni 
milioni 40. Jose alikuwa Uingereza kwa siku mbili na ndani ya siku hizi 
ndio jana walikubaliana na uongozi wa club ya chelsea kutia wino kwenye 
mkataba huo. Awali Jose alisema anakuja Uingereza kwenye mchezo wa 
Crystal Palace na Watford Uliofanyika Wembley Jumatatu Iliyopita Lakini 
ukweli ni kwamba alikuwa anakuja kwa ajili ya mkataba wake na Chelsea, 
Jose ameongelea kwa muda wa miezi minne sasa kuwa anakuja chelsea baada 
ya msimu kuisha so kama ulikuwa unasubiria sasa its official.
Jose mwenye miaka 50 atatangazwa 
rasmi wiki ijayo na washindi wa kombe la Europa ambao ni Chelesea. Game 
ya kwanza ya Mourinho itakuwa mchezo wa Kirafiki na club ya Thailand 
Singha All Stars XI, Baada ya hapo ana Game Malaysia na Indonesia.