| Mh Msigwa akishuka kwenye gari la polisi kuingia mahakamani | 
Mbunge  wa  jimbo la Iringa mjini 
mchungaji,  Peter Msigwa akishuka katika gari ya  polisi baada ya 
kufikishwa mahakamani mchana  huu katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa  
wa Iringa  pamoja na  watuhumiwa  wengine  zaidi ya 60 .
Ulinzi mkali 
uliwekwa katika eneo hilo la mahakama  kuzuia wafuasi  wa  
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuingia eneo la Mahakama jambo lililowafanya wafuasi hao kushindwa kushuhudia vyema kesi hiyo, inayomkabiri Mbunge wao, kwa vile walilazimika kushuhudia wakiwa nje ya geti
 Kada wa 
Chadema Frank Mwaisumbe akiingia na viongozi  wengine wa chadema 
mahakamani hapo huku  wafuasi  wao  wakizuiwa nje ya mahakama
 Wafuasi  wa
 Chadema  wakiwa  wamezuiliwa nje ya viwanja  vya mahakama kuu kanda  ya
 Iringa  wakati mbunge  alipofikishwa katika mahakamani   mchana  huu