Muandamanaji huyu alimkaribia ila alidhibitiwa vilivyo 
 
Raisi wa Urusi bwana Putin alipata bonge la mshangao 
wakati wa ziara yake ya Ujerumani baada ya waandamanaji kujitokeza. 
katika waandamanaji hao kulikuwa na wanawake watatu ambao walikuwa vifua
 wazi ambao walijitokeza nao mbele na kutaka kwenda kumkumbatia rais 
huyo.
 Bwana Putin alikuwa ameenda katika uzinduzi wa Hanover 
Messe industrial trade show yeye na mwenyeji wake Chancellor Angela 
Merkel ndipo walipojitokeza waandamanaji hao wakipinga sera na sheria za
 nchi yake juu ya mambo mbalimbali ambayo wao wanaona sio sawa
Akiliongelea hilo bwana Putin anasema alilitegemea ila 
anasema walinzi wa kijerumani walikuwa wakali sana kwa wamama hao kiasi 
cha kuwala wote chini kwa nguvu na muda mfupi kiasi kwamba hakusikia 
vizuri maneno waliyo yasema ila anasema alifurahishwa nao.
Pamoja na hayo kulikuwa pia na mabango kwenye mitaa hiyo ya miji ya Ujerumani. 
 |