
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limemtaka mshambuliaji Nsa Job wa Coastal Union kuwasilisha maelezo yake juu ya madai kuwa alipewa rushwa ya sh. milioni mbili ili asiifunge moja ya timu vigogo vya soka nchini.
Job
 alikaririwa Aprili 3 mwaka huu na kituo cha redio cha Clouds FM katika 
kipindi cha Amplifier kuwa alipewa kiasi hicho cha fedha na kiongozi wa 
timu husika ili asiifunge katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom, lakini 
alipokea fedha hizo na kuifunga timu hiyo.
Baadaye
 kiongozi huyo alikuwa akimtaka arejeshe fedha hizo. Pia TFF 
imekiandikia kituo hicho cha redio kutaka nakala ya kipindi hicho ili 
pamoja na maelezo ya mshambuliaji huyo vipelekwe katika Kamati ya 
Nidhamu kwa ajili ya hatua za kinidhamu.