Rais 
Jakaya Kikwete akimpongeza Rais Mpya wa Jamhuri ya Kenya Mheshimiwa 
Uhuru Kenyatta huko Ikulu mara baada ya kuapishwa rasmi kuwa rais wa nne
 wa nchi hyo katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa kimataifa wa 
michezo wa Moi-Kasarani jijini Nairobi jana tarehe 9.4.2013.
Rais Mpya
 wa Kenya, Uhuru Kenyatta akiwashukuru Marais na wakuu wa nchi 
waliohudhuria sherehe za kumwapisha wakati wa dhifa ya kitaifa 
aliyoiandaa huko ikulu jijini Nairobi.
Rais wa 
Kenya aliyemaliza muda wake, Mwai Kibaki akifanya mazungumzo na Rais 
Jakaya Kikwete na Mkewe Mama Salma huko Ikulu mara baada ya sherehe ya 
kumuapisha Rais mpya wa Jamhuri ya Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyatta 
kukamilika.
Mke wa 
Rais Mama Salma Kikwete akifanya mazungumzo na wake wa viongozi wa juu 
wa Kenya, Mama Magrate Kenyatta (kushoto) ambaye ni mke wa Rais Uhuru na
 Mama Recheal Ruto (kulia) Mke wa Naibu Rais wa nchi hiyo Mheshimiwa 
William Ruto huko ikulu jijini Nairobi mara tu baada ya kuapishwa 
viongozi hao jana tarehe 9.4.2013.
Rais wa 
Kenya aliyemaliza muda wake, Mheshimiwa Mwai Kibaki akifanya mazungumzo 
na Rais Jakaya Kikwete na Mkewe Mama Salma huko Ikulu mara baada ya 
sherehe ya kumuapisha Rais mpya wa Jamhuri ya Kenya Mheshimiwa Uhuru 
Kenyatta kukamilika.
Mke wa 
Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na Mke wa Rais wa Jamhuri ya Kenya 
Mama Magrate Kenyatta katika ikulu ya Kenya jijini Nairobi mara baada ya
 sherehe za kuwaapisha kukamilika. 





