NDEGE YA MAREHEM WAKILI NYAGA YAANGUKA ARUSHA NA KUUA
Ndege iliyokuwa inamilikiwa na Wakili Maarufu Marehem Nyaga Mawalla aliyefariki wiki tatu zilizopita na kuzikwa Nairobi, imeanguka ikiwa katika hatua za mwisho za kutua katika uwanja wa Ndege wa Arusha Taarifa
zinasema kuwa ndege hiyo ilikuwa na rubani pekee anayejulikana kwa jina
la Jamal B S, au maarufu kama "Bob Sambeke" aliyekuwa anatokea West
Kilimanjaro ambaye naye kapoteza maisha (kafariki)! Inadaiwa kuwa ndege hiyo ilijaribu kutua baada ya masaa ya kawaida ya kufunga kiwanja (saa 12.30 jioni) kupita.