![]()  | 
| Ridhiwani Kikwete akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kutambulishwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya ujenzi wa eneo la Mafia | 
Mwenyekiti
 wa klabu ya Young Africans Sports Club alhaj Yusuf Manji leo 
amemtambulisha wakili Ridhiwani Kikwete kuwa mwenyekiti wa kamati ya 
ujenzi wa kitega uchumi katika eneo la klabu lililopo makutano ya 
Mafia/Nyamwezi  eneo la Ilala jijini Dar es salaamAkiongea na waandishi wa habari leo makao makuu ya klabu Manji 
amesema uteuzi wa Ridhiwani umezingatia uwezo wake kwa taaluma yake, na 
moyo alionao katika kujitolea katika kazi mbali mbali za klabu ya Yanga"Wote
 tunamfahamu Ridhiwani amekua ni mwanachama wa Yanga kwa muda mrefu, 
amekua akijitoa katika kazi mbali mbali za maendeleo ya klabu, hivyo 
tumeona ni vizuri kumpa fursa hiyo ili aweze kusaidia katika kuleta 
maendeleo ya klabu" alisema Manji
Katika kamati hiyo ambayo 
Ridhiwani ameteuliwa , amepewa fursa ya kuteua/kuchagua wajumbe 
atakaoshirikiana nao katika ujenzi wa kitega uchumi hicho katika mtaa wa
 mafia, pia atakua na uwezo wa kuongeza wajumbe au kupunguza kulingana 
na mahitaji kwa kipindi hicho.
Mara baada ya kutambulishwa kwa 
wanachama na waandishi wa habari, Ridhiwani alisema anashukuru kwa 
mwenyekiti wa klabu ya Yanga Manji kumteua kushika nafasi hiyo na 
kuahidi kuwa atajitahidi kadri ya uwezo wake kuhakikisha ujenzi huo 
unafanikiwa.
 "Nitakaa na kuangalia ni wajumbe gani ambao tutaweza
 kukaa pamoja na wajenzi (wakandarasi) ili kuweza kufanikiwa katika 
ujenzi wa kitega uchumi, kwani napenda eneo hilo liwe sehemu ambayo 
litasaidia katika uchumi wa klabu" alisema Rdihiwani 
Aidha
 Ridhiwan aliendelea kusema kuwa Kiwanja cha mafia kimekuwepo kwa mda 
mrrefu bila ya kufanyiwa muendelezeo, ila naamini tutajitahidi ili 
kuweza kuhakisha historia inajengwa kwa kubadili eneo hilo na kuwa 
sehemu ya kivutio na ya kuiingiza pesa klabu.
Ridhiwani mwisho 
alimalizia kwa kusema hawataishia katika ujenzi wa kiwanja cha mafia tu 
bali wataweka mipango kuhakikisha kuwa hata katika matawi ya Yanga 
sehemu mbali mbali wanaweza kuwekeza na kujenga majengo ambayo 
yatasaidia katika kuendeleza uchumui wa klabu. 

