
Kamanda wa Polisi
 Kanda Maalum Dar es Salaam Suleiman Kova (kushoto) akizungumza na 
vyombo vya habari jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kamanda wa Polisi mkoa 
wa Kinondoni ACP Charles Kenyela.
Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam linawashikilia watu wanne kwa tuhuma za kujishughulisha na uchochezi wa kidini.
Watu hao 
wamekamatwa hivi karibuni katika msako maalum unaoendeshwa na Jeshi la 
Polisi Kanda Maalum katika hali ya kukabiliana na uchochezi wa kidini 
ambao lengo lake ni kuleta chuki pamoja na ubaguzi wa kidini
Kamanda wa 
Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam Suleimani Kova amewataja watu hao kuwa
 ni Kombo Hassan Zuberi mkazi wa Mburahati Barafu (32), Basote Hassan 
Tandala Rayan mkazi wa Gongo la mboto (24), Mohamed Hassan Sharif mkazi 
wa Tabata Bima(33) na Salum Athman Mahambi mkazi wa Tunduma(46).
Aidha Kamanda 
Kova ametoa onyo kali kwamba Jeshi la Polisi halitasita kuwachukulia 
hatua wale wote wanaoleta uchochezi kupitia shughuli za kidini au 
kisiasa.
SOURCE:DJ-SEK