UONGOZI
wa Klabu ya Simba umethibitisha kuwa mshambuliaji wa timu hiyo, Felix
Sunzu hatokuwamo kwenye msafara wa timu hiyo utakaoelekea Arusha kesho
kwa ajili mechi ya ligi dhidi ya JKT Oljoro.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam msemaji wa Simba, Ezekiel Kamwaga alimesema kuwa
Sunzu ameondolewa katika kikosi kitakachoivaa JKT Oljoro kutokana na
kuwa majeruhi.
"Kama tulivyopanga awali kikosi chetu kitaondoka kesho kuelekea Arusha kikiwa na wachezaji 20.
"Mpaka
wakati huu mchezaji ambaye ninaweza kukuthibitishia kwamba hatokuwa
miongoni mwa wale watakaosafiri ni Felix Sunzu ambaye bado anasumbuliwa
na majeraha,".alisema Kamwaga.
Kamwaga
alisema kuwa, orodha kamili ya wachezaji 20 watakaosafiri kuelekea
Arusha ilitarajiwa kutangazwa mapema baada ya kumalizika kwa pambano
kati ya Timu ya Taifa(Taifa Stars) na Cameroon leo jioni.
"Nani
na nani watakuwamo katika kikosi kitakachosafiri itajulikana leo
jionibaada ya mechi kati ya Taifa Stars na Cameroon kama unavyojua tuna
wachezaji kwenye timu ya Taifa. Hatuwezi kujua kuna nini kitatokea baada
ya mchezo,".alisema Kamwaga.
Pambano baina ya Simba na JKT litapigwa Jumamosi hii kwenye Dimba la Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
Katika
pambano la mzunguko wa kwanza lililopigwa kwenye Uwanja wa Taifa
jijini Dar es Salaam, Wekundu wa Msimbazi, Simba ilichomoza na ushindi
wa mabao 4-1