Mamlaka
 ya Bandari Tanzania (TPA) imeongeza ukusanyaji wa mapato katika bandari
 ya Dar es Salaam kutoka shilingi bilioni 28 mwezi Novemba hadi shilingi
 bilioni 50 (dola milioni 18 hadi dola milioni 31) katika mwezi wa 
Disemba, kufuatia kusimamishwa kwa muda maofisa 16 wa bandari wanaotuhumiwa kwa mwenendo usiofaa.
Maofisa 
hao wa bandari, wakiwemo wakurugenzi wa ngazi za juu, walisimamishwa kwa
 muda mwezi Disemba baada ya Wizara ya Usafirishaji kuanzisha uchunguzi 
wa ndani kwa lengo la kutoa mwitikio wa malalamiko ya wateja kuhusu 
kucheleweshwa katika bandari hiyo, kwa mujibu wa Waziri wa Usafirishaji 
Harrison Mwakyembe.
Maofisa wa bandari wengine wasiopungua sita.
 Uchunguzi huo, ambao bado unaendelea, uligundua kuwa waajiriwa wa 
bandari walibadilisha mwelekeo wa biashara kutoka katika bandari kwenda 
kwa kampuni ndogo za usafirishaji na utoaji mizigo wanazomiliki, 
ukiukaji wa moja kwa moja wa mkataba wao wa ajira.
"Wateja 
wanakimbia bandari yetu kwa sababu ya ucheleshaji wa kukusudia 
unaofanywa na waajiriwa wasio na maadili ambao wanaongeza gharama za 
kufanya biashara," Mwakyembe aliiambia Sabahi. "Hii ni kinyume na 
mikataba yao ya ajira na wana mgongano wa maslahi na mwajiri wao ambae ni Serikali."
Miongoni 
mwa viongozi wa bandari wa ngazi ya juu waliosimamishwa ni Mkurugenzi 
Mkuu wa TPA Ephraim Mgawe, Mkurugenzi wa Mipango Florence Nkya, 
Mkurugenzi wa Uhandisi Bakari Kilo, Mkurugenzi wa Mifumo ya Utawala 
Maimuna Mrisho, Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Ayub 
Kamili, Naibu Mkurugenzi Mkuu Hamad Koshyuma, Naibu Mkurugenzi Mkuu 
Julius Fuko, na Meneja wa Bandari Cassian Ng'amilo.
Mashtaka 
rasmi bado hayajatolewa dhidi ya viongozi waliosimamishwa na bado 
hawajajibu tuhuma zozote hadharani. Mwakyembe alisema Bodi ya 
Wakurugenzi ya TPA itakutana hivi karibuni kutoa uamuzi wa mwisho 
kuhusiana na ajira yao.
![Meli zinapakua makontena katika bandari ya Dar es Salaam tarehe 29 Disemba, 2012. [Deodatus Balile/Sabahi]](http://sabahionline.com/shared/images/2013/01/07/tanzania-dar-port-340_227.jpg)