CHADEMA imesema imelazimika kuratibu maandamano na mkutano wa hadhara
kama ishara ya kuwapokea wabunge wa upinzani kwa madai ya kuwashitakia
Wananchi kitendo cha Bunge kuondoa kwa hoja zao binafsi.
Moja
ya h oja hizo ni hoja binafsi ya Mnyika iliyokuwa ikipendekeza Bunge
lijadili na kupitisha maazimio ya hatua za haraka za kuboresha
upatikanaji wa maji safi na ushughulikiaji wa maji taka katika jiji la
Dar es Salaam, hoja ambayo ilitupiliwa mbali na kuzua mtafaruku bungeni.
Hoja
nyingine ni ya Mbunge wa Kuteuliwa na Rais, ambaye pia ni mwenyekiti wa
NCCR-Mageuzi, James Mbatia aliyoitoa bungeni juu ya udhaifu wa mitaala
ya elimu nchini.
Jeshi la Polisi nchini
kupitia Kamanda wa Polisi wa mkoa Kipolisi wa Temeke, Engelbert Kiondo
amesema ni marufuku kwa CHADEMA kuandamana kama walivyokusudia ila, ni
ruhusa kufanya mkutano.
Amesema sababu
za kuzuia maandamano hayo ni kutokana na usumbufu utakaojitokeza katika
maeneo ambayo maandamano hayo yamepangwa kupitia ikiwa ni pamoja na
kuingilia na pengine kuzuia shughuli za kawaida za maeneo hayo, matumizi
ya barabara na pengine kuchangia vitendo vya uharibifu wa mali na
uvunjifu wa amani. Hivyo akasema alikwishakuwasiliana na viongozi wa
CHADEMA wa Temeke kuhusu suala hilo na kuwataarifu kuwa maandamano
yoyote yatakayofanyika yatakuwa ni kinyume na sheria na hivyo
itawalazimu Polisi kuchukua hatua za kisheria pale inapobidi.
Naye
Kamanda wa CHADEMA anayeratibu maandamano hayo, Benson Kigaila alisema
maandalizi ya maandamano hayo yanaendelea kama yalivyopangwa kutokana na
kuwa hajapokea ujumbe wowote kutoka Jeshi la Polisi kama walivyoahidi
kumpigia simu kwa maelezo zaidi.
Maandamano hayo yamepangwa kufanyika kuanzia TAZARA na kuhitimishwa kwa mkutano wa hadhara wilayani Temeke.
Benson
alisema mkutano huo ni mwanzo wa mfululizo wa mikutano itakayofanyika
kwenye kanda 10 zilizotengwa na CHADEMA, kuanzia mwenzi huu.