Mabingwa wa soka Tanzania Bara,Simba wameshindwa kutamba mbele ya
Wenyeji wao mara baada ya kufungwa mabao 3-1 katika mechi ya kirafiki
dhidi ya timu ya Taifa ya Jeshi la Oman. mechi hiyo ilichezwa Ijumaa
jioni kwenye uwanja wa Qaboos Complex jijini Muscat.
bao la simba
lilifungwa katika kipindi cha pili na Haruna Moshi 'Boban' huku
Mwenyekiti wa Simba,Ismail Aden Rage akiwa jukwaani pamoja na viongozi
wengine wa simba, Rahma Al Kharoos na Musleh Rawahi pamoja na Kocha
Talib Hilal wakiishuhudia Simba ikizama mbele ya wanajeshi hao
Mwenyekiti wa Simba na Mfadhili wa safari ya Simba Rahma Al Kharoos akiangalia timu ya Simba ikipokea kichapo