Mdhamini
 wa safari ya Simba Rahma jana aliwaalika Simba nyumbani kwake eneo la 
Al Kheri jijini Muscat, Oman jana usiku kwa ajili ya chakula cha usiku.  
Walikula pamoja na baadaye bendi maalum kutoka Tanzania iliwapigia 
muziki na wakaserebuka pamoja huku Rahma akimwaga noti kama maji.
  Katika
 hafla hiyo, Rahma alikabidhiwa jezi ya Simba na Musleh Rawah ambaye ni 
mmoja wa wadau wa Msimbazi na jezi ya timu ya taifa ya Oman na kocha wa 
makipa wa timu hiyo, Haroun Amur. |