Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha,Kamishna Msaidizi wa Polisi
(ACP),Liberatus Sabas (kulia) akiongea na Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya
jinai Mkoa wa Arusha Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP),Camirius
Wambura aliyeshika madawa ya kulevya aina ya mirungi nje ya jengo la
Makao Makuu ya jeshi hilo Jijini Arusha mara baada ya kukamata shehena
hiyo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha,Kamishna Msaidizi wa
Polisi (ACP),Liberatus Sabas (wa pili kushoto) akiongea na baadhi ya
Waheshimiwa Madiwani na Waandishi wa habari nje ya jengo la makao makuu
ya jeshi la Polisi Jijini Arusha.
Gari aina ya Fuso lenye namba za usajili T. 284 AGL ambalo
lilikuwa na shehena ya mirungi viroba vipatavyo 173 vyenye jumla ya
uzito wa kilogramu 1800.(Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi
Arusha).