
 Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye  
---
SIKU
 moja baada ya Baraza la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo 
(Bavicha), kudai CCM inashirikiana na baadhi ya viongozi wake kukisaliti
 chama hicho, Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amekanusha tuhuma
 hizo.Nape alisema CCM haihusiki na mgogoro wowote ndani ya chama hicho,
 hivyo wanapaswa kumtafuta mchawi wao siyo kukilaumu chama chake.
“Mchawi
 wanaye wenyewe ndani ya chama chao, hatuhusiki na lolote hivyo 
wanapaswa kujipanga na kuulizana kubaini tatizo linalowasumbua,” 
alisema.
Aliongeza kuwa CCM haina muda wa kuhujumu chama hicho, ila wana muda wa kutekeleza ilani za chama maeneo mbalimbali nchini.
Nape alisema kutokana na hali hiyo, CCM imejipanga kuhakikisha ahadi zinatekelezwa kwa vitendo, ikiwamo maazimio yaliyotolewa kwenye mkutano mkuu wa chama hicho.Baadhi ya viongozi wa Bavicha wanaodaiwa kushirikiana na CCM kudhooficha Chadema na wengine walifukuzwa uanachama