Wahandisi wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) wakikamilisha
kufunga kioo kipya ambacho kimenunuliwa kutoka nchini Marekani cha
ndege yao aina ya Dash-8 Q300 yenye namba za usajili SH-MWF ambayo
ilipata ufa (Wind shield crack) tarehe 11 Januari, 2013, muda mfupi
baada ya ndege hiyo kuruka kutoka Kigoma kurudi Dar Es Salaam katika
safari zake za kawaida. Matengenezo
hayo yanafanyika katika uwanja wa ndege wa Kigoma yakisimamiwa na
Mhandisi Righton Mwakipesile na Mhandisi Merkior Karwani. Uongozi
wa ATCL umedhibitisha kuwa safari za Dar-Kigoma-Dar zitaendelea kama
ratiba yao inavyoonyesha punde kuanzia kesho tarehe 22/1/2013.