Habari ifuatayo imetumwa na Abunuwasi Alinacha (email: a...a...@gmail.com):
---
Katibu
 Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe. Wilbroad Slaa 
majuzi, Ijumaa, kule Sikonge, Tabora amezua na kutunga jipya.
Amedai
 kuwa Julai 2, mwaka huu, 2012, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete alisafiri kwenda Hong Kong kumwokoa 
mtoto wake wa kiume, Ridhiwani Kikwete ambaye anadaiwa kuwa alikuwa 
amekamatwa na mihadarati siku moja kabla, yaani Julai Mosi.
Huu ni uongo wa dhahiri kwa sababu ratiba ya Mhe. Rais Kikwete katika siku hizo anazozitaja Slaa iko wazi.
Julai
 Mosi, akitumia Ndege ya Rais, alisafiri kwenda Rwanda ambako 
alihudhuria Sherehe za Miaka 50 ya nchi hiyo na akalala mjini Kigali. 
Julai 2 alisafiri kwenda Bujumbura kuhudhuria Sherehe za Miaka 50 ya 
Burundi.  Alirejea Dar es Salaam Julai 3 na Julai 4 alikutana na ujumbe 
wa Kampuni ya IBM na Mjumbe Maalum kutoka Zimbabwe. Julai 5, alikwenda 
Dodoma ambako aliendesha Kikao cha Baraza la Mawaziri na kurejea Dar es 
Salaam siku hiyo hiyo. Sasa alikwenda Hong Kong lini? Ama alikuwa 
Burundi na Hong Kong siku hiyo hiyo? Slaa anadai pia kuwa alipowasili 
Hong Kong, Mheshimiwa Rais Kikwete alipokelewa na Balozi wa Tanzania 
nchini China, Mheshimiwa Philip Marmo ambaye alimpeleka kwenye mkutano 
na Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Mheshimiwa Hu Jintao. Huu ni uongo 
mwingine wa dhahiri na ambayo sijui unamsaidia nini Slaa. Slaa anasema 
uongo kuhusu Balozi Marmo kwa sababu ratiba ya Mheshimiwa Marmo kwa siku
 sita za mwezi Julai nayo iko wazi na siyo kificho.
Kwanza,
 Ubalozi wa Tanzania katika China hauko Hong Kong bali uko mjini Beijing
 na Mheshimiwa Marmo hajawahi hata kufika Hong Kong. Taarifa kutoka Hong
 Kong amekuwa anazipata kutoka kwa Balozi Mdogo wa heshima wa Tanzania 
Mheshimiwa Clement Chan. Hata juzi, Ijumaa, Oktoba 26, Balozi Marmo 
alikutana na Bwana Clement Chan. Balozi Marmo anapanga kutembelea Hong 
Kong kwa mara ya kwanza mwishoni mwa mwezi ujao, Novemba, 2012. Angalia 
ratiba ya Mheshimiwa Marmo katika wiki ya kwanza ya mwezi Julai mwaka 
huu:
Julai Mosi, Balozi Mamro alikuwa 
ofisini Beijing. Julai 2, Balozi alihudhuria Sherehe za Siku ya Mongolia
 mchana na usiku alihudhuria Sherehe za Siku ya Djibouti kwenye Hoteli 
ya Lengedane mjini Beijing. Siku nzima ya Julai 3 alishiriki katika 
warsha ya Kampuni ya China Chemicals Techonologies Group ambayo inataka 
 kufungua viwanda cha madawa na mbolea nchini Tanzania. Asubuhi ya Julai
 4, Balozi Marmo alikutana na ujumbe wa Kampuni ya Sichaun Honda Group 
inayowekeza katika miradi ya Mchuchuma na Liganga na jioni ya siku hiyo 
alikutana na ujumbe wa Kampuni ya Mawasiliano ya ZTE. Julai 5, Balozi  
alihudhuria Sherehe za Siku ya Venezuala Day na Julai 6 alijiunga na 
Mabalozi wa Nchi za Jumuia ya Afrika Mashariki katika mkutano wa Forum 
on Trade na Cooperation na jioni alihudhuria Sherehe za Rwanda Day. 
Sasa, Balozi Marmo alikwenda lini Hong Kong kumpokea Mheshimiwa Rais 
kama siyo uongo?
Katika
 siku zinazotajwa, Bwana Ridhiwan alikuwa Dar es salaam muda wote.  Kwa 
hakika, Ridhiwan hajapata kufika Hong Kong ama China katika maisha yake 
yote. Nchi pekee inayokaribia China ambayo amewahi kuitembelea ni Dubai 
kwa sababu hata India hajapata kufika. Ratiba hizi za Mhe. Rais na 
Mheshimiwa Marmo na ukweli kuwa Ridhiwan hajapata hata kufika China ama 
Hong Kong ni ushahidi usiopingika kuwa Mzee Slaa kwa mara nyingine 
ametunga, yeye amekuwa bingwa wa goofing. Huyu ni mtu anayezeeka vibaya.
 Tunaamini kuwa ameanza kuchanganyikiwa pengine kwa kuzidiwa na jukumu 
ya kulea mtoto-mjukuu na kumtunza mchumba Bi Josephine ambaye wanaishi 
kama vimanda kwa sababu huyo mama bado anayo ndoa halali. Pole sana Mzee
 Slaa kama Josephine na mwanae amekushinda
MAMLAKA 
ya Chakula na Dawa (TFDA) imewekwa matatani ikielezwa kuwa nayo 
inastahiki kuchukuliwa hatua kutokana na kuzembea katika ukaguzi wa dawa
 na hivyo kusababisha dawa bandia za kupunguza makali ya ukimwi (ARV’s) 
kusambazwa.
Sakata hilo linakuja wiki chache tangu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Hussein Mwinyi, kumsimamisha kazi Mkurugenzi wa Bohari ya Dawa (MSD), Joseph Mgaya, na viongozi wengine kupisha uchunguzi wa tuhuma za kusambaza dawa hizo.
Wengine waliosimamishwa kazi ni mkuu wa kitengo cha udhibiti ubora na ofisa uthibiti ubora huku kiwanda cha dawa cha Tanzania Pharmaceutical Industries Ltd (TPI) kikisitishiwa uzalishaji na usambazaji wa dawa zilizokwishatengenezwa.
Taarifa za ndani ya TFDA ambazo Tanzania Daima imedokezwa na mmoja wa maofisa wake ambaye aliomba kuhifadhiwa jina kwa vile si msemaji, zilisema kuwa mamlaka hiyo nayo ilizembea katika sakata zima la dawa bandia za ARV’s kusambazwa.
Kiwanda chochote kabla ya kuzalisha dawa au chakula ni lazima kipate kibali cha TFDA baada ya kukaguliwa na kukidhi viwango husika.
“Hata dawa ingekuwa inaingizwa kutoka nje ya nchi, vilevile TFDA inapaswa kukikagua kiwanda husika kuona kama kina ubora wa kutengeneza dawa na kukidhi viwango,” kilisema chanzo chetu.
Gazeti hili pia limefanikiwa kupata nakala ya waraka wa TFDA kuhusu hali ya viwanda vya dawa nchini, ambayo inabainisha kuwa Tanzania ina viwanda saba vya dawa vilivyosajiliwa katika mwaka 2011/2012.
Viwanda hivyo ni Shelys Pharmaceuticals Ltd, Zenufa Laboratories Ltd, Mansoor Daya Chemicals Ltd, Keko Pharmaceuticals (1997) Ltd, Tanzania Pharmaceutical Industries Ltd, A.A. Pharmaceuticals Ltd na Tanzansino United Pharmaceuticals (T) Ltd.
Waraka huo unabainisha kuwa kiwanda cha Tanzansino United Pharmaceuticals (T) Ltd, ambacho serikali kupitia Jeshi la Kujenga Taifa ni mmbia mmojawapo kimesimamisha utengenezaji dawa tangu Agosti 2010 kutokana na mwekezaji wa nje kujiondoa.
“Ukaguzi uliofanywa na TFDA katika miaka ya fedha ya 2010/11 na 2011/12 umeonyesha kuwa hakuna kiwanda kilichokidhi viwango vya utengenezaji wa dawa,” alisema ripoti yao.
TFDA katika taarifa yake hiyo inakiri kuwa viwanda vya dawa hapa nchini katika kipindi cha miaka miwili iliyopita vimeshindwa kukidhi vigezo vya usajili wa dawa.
Kutokana na hali hiyo dawa za viwanda hivyo zimekuwa zikiruhusiwa na mamlaka hiyo kuwepo sokoni kwa kuzingatia utaratibu maalumu ambao hauzingatii vigezo vyote vya usajili wa dawa.
“Utaratibu huu ulikuwa wa muda mfupi uliokuwa na nia ya kutoa muda kwa kiwanda husika kurekebisha mapungufu ili dawa zao zisajiliwe. Baadhi ya dawa zinazotengenezwa na viwanda vya ndani ni za tiba za ugonjwa wa malaria na vijiua sumu,” iliongeza taarifa.
Pia inafafanua kuwa katika siku za karibuni, sampuli za matoleo (batches) kadhaa za dawa za viwanda hivyo zilizochukuliwa katika soko na kuchunguzwa zimeonekana kuwa na ubora duni na hivyo kuondolewa.
Ni katika mtiririko huo, mtoa habari wetu anasema TFDA haijawahi kutoa kibali kwa kiwanda cha TPI kuzalisha dawa za ARV’s kinachoonyesha kuwa kiwanda hicho kimekidhi vigezo tajwa.
Lakini katika hali inayoonyesha kutokuwepo umakini, TFDA ilizisajili dawa hizo za ARV’s kutoka TPI wakati katika ripoti yake wanakiri kuwa kiwanda hicho hakina sifa za kuzizalisha.
“Dawa inaweza kuwa moja lakini ikawa na matoleo tofauti, hivyo hata toleo hilo la dawa bandia zinazolalamikiwa halikuletwa TFDA kwa ukaguzi maana ingebainika haraka kabla ya kuingia sokoni,” kiliongeza chanzo hicho.
Ofisa huyo anashauri kuwa TFDA ilipaswa kuwa na mkaguzi wake ndani ya MSD ambaye angekuwa anasaidia kukagua na kuhakikisha dawa hizo hazizalishwi na kusambazwa.
“Hapa utaona kuwa haikuwa sahihi kumwajibisha mkurugenzi wa MSD pekee na kutuacha TFDA ambao hatukutimiza wajibu wetu. MSD hawana utaalamu wa kuchunguza dawa bandia hiyo ni kazi ya TFDA,” alisisitiza ofisa huyo.
Dawa hiyo bandia aina ya TT-VIR 30 toleo namba OC.01.85 iliyotengenezwa Machi 2011 na kuisha matumizi Februari 2013, nyaraka zake zilionyesha kiwanda cha TPI kiliwauzia MSD.
Waziri Mwinyi alieleza kuwa vidonge vilivyokutwa kwenye vifungashio vya dawa husika vilikuwa vimesajiliwa na TFDA.
Mkurugenzi Mkuu wa TFDA jana alipotafutwa kwa njia ya simu, alisema atatoa ufafanuzi wake leo akiwa ofisini.