Watu  mbalimbali wakiwa wamelizunguka jenereta Jana usiku.

  Mwanamuziki
 kutoka DRC-Congo,JB Mpiana akitumbuiza jukwaani mara baada ya kupanda 
mnamo majira ya saa tisa kasoro,baada ya hitilafu za umeme kwenye 
jenerata kurekebishwa.
SHOO YA 
UZINDUZI WA ALBAM YA PILI YA MASHUJAA BAND, ILIINGIA DOSARI NA KUTAKA 
KUSHINDWA KUFANYIKA  KATIKA VIWANJA VYA LEADERS CLUB USIKU HUU KUTOKANA 
NA KATIZO LA UMEME LA MARA KWA MARA LINALOSABABISHWA NA JENERETA 
LINALOTUMIWA KUTOA UMEME KATIKA VIWANJA VYA LEADERS CLUB,JIJINI DAR.
HALI HIYO IMEPELEKEA MMILIKI WA BENDI YA MASHUJAA,MAMA SAKINA KUPOTEZA FAHAMU NA KUKIMBIZWA HOSPITALI.
HADI SASA HAIJAFAHAMIKA KUWA HALI YAKE IKO VIPI KWANI HAKUNA TAARIFA ZOZOTE JUU YAKE.
MAFUNDI 
BADO WANAENDELEA NA MAREKEBISHO YA JENERETA HILO NA IWAPO LITAKAA 
SAWA,BASI NI MOJA KWA MOJA BENDI YA WENGE BCBG NDIO ITAPANDA 
JUKWAANI,CHINI YA MKONGWE JB MPIANA.
