| Maghala ya kuhifadhia bidhaa mbali mbali za wafanya biashara wa mwanjelwa Mbeya yameteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo maghala hayo yapo maeneo ya uwanja wa ndege wa mwanjelwa | 
| Wanausalama wakiwa makini na vibaka ambao walitaka kuvamia eneo hilo la moto kutaka kupora mali kujifanya wanaokoa mali hizo | 
| Moja ya gari ya kampuni ya jambo ikiungua moto katika maghala hayo | 
| Moja ya wafanyabiashara hao ambaye anamizigo yake katika maghala hayo akikatazwa na mwanausalama kwamba asiende kmuokoa mali zake kwani moto ni mkubwa awaachie kikosi cha zimamoto kifanye kazi yake | 
| Mfayabiashara huyo haamini mcho yake huku akilia akiona bidhaa zake zikiteketea kwamoto | 
| Kama kawaida kmufa kmufaana hapa vibaka wakigombea sahani na masufuria kwenye box | 
| Kwakweli ilikuwa hatari kwani vibaka walikuwa wanarusha mawe kwa polisi na kwa baadhi ya magari hapa hili gari ikitoka katika ghala hilo likiwa limevunjwa kioo cha mbele | 
| Baadhi ya wananchi wengi wakiwa katika tukio hilo | 
| Haya si maji bali ni mafuta ya kula ambayo yamemwagika baada ya blastiki kuyeyuka kwa moto | 
| Asubuhi hii moto ndiyo unaishia | 
| Hali halisi baada ya kuungua kwa maghala hayo hili si tope mali ni mafuta ya kula yaani mafuta ya kupikia | 
| Baadhi ya wafanyabiashara wakijaribu kuokota baadhi ya mabaki ya bidhaa zao zilizopona katika moto huo | 
| Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza kamanda diwani |