Jarida la Forbes ambalo mara 
nyingi limekua likitoa ripoti za matajiri wa dunia na utajiri wao 
limesema tajiri wa Tanzania Said salim Bakhresa ambae ameshika namba 30 
kati ya matajiri 40 wa Afrika aliacha shule akiwa na umri wa miaka 14 na
 kuanza kuuza potato mix baada ya hapo akafungua restaurant ndogo lakini
 leo ameajiri zaidi ya watu elfu mbili kwenye kampuni yake.
Kampuni hii ndio kampuni inayoongoza kwa kutengeneza unga wa ngano Afrika Mashariki na kati ambapo kwa siku inatoa tani 3,200.
