Simba ikipambana na Mthare United katika uwanja wa Shekh
Abeid huko Arusha. Imeibuka na ushindi wa gili 2 kwa 1.Mchezo huu ni wa kirafiki kati ya timu hizi, Simba
ikijiandaa na ligi kuu ya Tanzania.
Simba inacheza mechi hiyo
kutokana na maombi ya kocha wake Mkuu Milovan Cirkovic, kutaka kuona
wachezaji wake ambao wamesajili hivi karibuni.
Simba inawakilisha
nchi kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika huku Azam ikishiriki
michuano ya Kombe la Shirikisho kwa kushika nafasi ya pili.