Kampuni
 ya Mawakili ya MALETA & NDUMBARO ADVOCATES, ambayo inawakilisha 
vilabu 13 vya LIGI KUU YA VODACOM TANZANIA, inapenda kutoa tamko kwa 
umma kama ifuatavyo:
Kampuni
 ya MALETA & NDUMBARO ADVOCATES, iliteuliwa na vilabu 13 vya LIGI 
KUU YA VODACOM TANZANIA, kwa maandishi, ili kuwawakilisha na kuwatetea 
katika kudai haki zao ambazo tayari SHIRIKISHO LA SOKA TANZANIA (TFF) 
liliamua kukata fedha za udhamini na viingilio vya mechi pasipo kuwashirikisha. 
 
Dk. Damas Daniel Ndumbaro, wakili mwandamizi, ndiye 
aliyekabidhiwa file hilo kwa mujibu wa utaratibu wa ofisi yetu.
Kwamba,
 tarehe MALETA & NDUMBARO ADVOCATES, kupitia wakili wake mwandamizi,
 Dk. Damas Daniel Ndumbaro, iliandika barua ya madai (Demand Notice) TFF
 na kuongea na waandishi wa habari.
 
Kwamba Mheshimiwa Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo,
 Mh. Juma Nkamia (MB) aliitisha mkutano kati ya TFF (ambayo 
iliwakilishwa na Wilfred Kidau-Mjumbe Kamati ya Utendaji, na Selestine 
Mwesiga, Katibu Mkuu), Bodi ya Ligi, Vilabu vya Ligi Kuu ya Vodacom 
Tanzania na Dk. Damas Daniel Ndumbaro (kama wakili wa vilabu). 
 
Mwenyekiti wa Mkutano huo, Mh. Juma Nkamia alitoa fursa kwa TFF, Bodi ya
 Ligi, na Wakili wa vilabu kutoa maelezo yao na hatimaye Mh. Juma Nkamia
 alitoa maelekezo kama ifuatavyo:
 
Jamal Malinzi sio Rais wa Nchi, na aliwaagiza wawakilishi wa TFF wafikishe ujumbe huo kwa Bw. Jamal Malinzi. Makato ya Tshs. 1000/= kwa kila tiketi ni wizi wa mchana.TFF isitishe makato ya 5% na Tshs. 1000 kwa kila tiketi mpaka watakapoongea na kukubaliana na vilabu.
 
Baadaya
 hapo, MALETA & NDUMBARO ADVOCATES, ilikutana na vilabu ambayo 
vilikuwepo siku hiyo na kukubaliana kuwa sasa tusibiri majadiliano na 
TFF na kwamba MALETA & NDUMBARO ADVOCATES, ikiongozwa na Dk. 
Ndumbaro iandae mapendekezo ili yajadiliwe na mkutano mkuu wa vilabu.
 
Kwamba
 tarehe 11 Oktoba 2014 TFF ilifanya mkutano wa Kamati ya Utendaji na 
kutoa tamko kuwa kumekuwa na taarifa za upotoshaji kuhusu kanuni za ligi
 kuu na kwamba Sekretariati ya TFF imefungua mashtaka dhidi ya Dk. 
Ndumbaro ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya Ligi na Mwenyekiti wa Kamati ya 
Uchaguzi ya Klabu ya Simba.
 
Kwamba
 Kamati ya Utendaji ya TFF iliendelea kusema kuwa Kutokana na madai ya 
klabu kuhusu vipengele kadhaa vya Kanuni za Ligi Kuu 2014/15, Kamati ya 
Utendaji imepanga kukutana na viongozi wa klabu za Ligi Kuu siku ya 
Jumamosi, Oktoba 18 mwaka huu ili kuwasikiliza na kushauriana kuhusu 
changamoto za kikanuni na uendeshaji wa mashindano kwa ujumla na kwamba.
 
TFF
 imefanya kosa kumshitaki Dk. Ndumbaro kwa kofia ya Mjumbe wa Bodi na 
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi Simba kwasababu barua toka MALETA &
 NDUMBARO ADVOCATES, barua za vilabu 13 na taarifa kwa vyombo vya habari
 ilikuwa bayana kuwa Dk. Ndumbaro anawakilisha vilabu vya ligi kuu kama 
wakili toka kampuni ya MALETA & NDUMBARO ADVOCATES na wala sio 
mwakilishi wa Bodi au Mwenyekiti wa uchaguzi wa Simba kwasababu hakukuwa
 na uchaguzi wa Simba.
Kwamba
 TFF inakiri kuwa klabu za Ligi kuu zinapaswa kukutana na TFF kujadili 
kasoro za Kanuni za Ligi kuu. Hapa TFF inakiri kuwa haikukutana na 
vilabu katika mchakato wa kutunga kanuni hizi na kwamba kanuni hizo 
zinakasoro. Ifahamike kwamba hayo ndio madai ambayo vilabu kupitia 
MALETA & NDUMBARO ADVOCATES iliyapeleka TFF kwa maandishi.
Tarehe
 7 Oktoba 2014 TFF iliepeleka Mshtaka katika Kamati ya Nidhamu dhidi ya 
Dk. Ndumbaro. Kamati ya Nidhamu ilipanga kusikiliza Mashtaka hayo tare 
09 / 10 / 2014 saa 08: oo mchana, yaani siku mbili tu baadaya ya 
kuwasilishwa katika kamati ya nidhamu. Mashitaka hayo yalijaa 
ubabaishaji na chuki binafsi dhidi ya wakili wa vilabu 13 vya Ligi Kuu.
Kwamba
 TFF ililazimisha kusikiliza mashtaka hayo kwa haraka na dharura ya 
ajabu pasipo kuwepo Dk. Ndumbaro ambaye alitoa taarifa ya maandishi kuwa
 atakuwa safarini Nchini Marekani kikazi, kwa barua ya tarehe 8th 
October 2014.
Kwamba
 Kamati ya Nidhamu ya TFF ilitoa maamuzi ya kumfungia Dk. Ndumbaro 
asijihusishe na Soka kwa kipindi cha miaka saba pasipo kutoa sababu za 
msingi za kufanya hivyo wala kutoa nakala ya hukumu hiyo.
Kwamba MALETA & NDUMBARO ADVOCATES kwa niaba ya vilabu vya Ligi kuu inapinga adhabu hiyo ya uonevu kwa misingi ifuatayo:-
Kamati
 ya nidhamu ya TFF haina mamlaka ya kisheria ya kushughulikia suala 
hili. (ARTICLE 2, 3,76 and 77 of TFF Disciplinary Code) Kamati
 ya nidhamu ya TFF ilikosea kuamua suala hili bila kutoa haki ya msingi 
ya kuisikiliza MALETA & NDUMBARO ADVOCATES na Dk. Damas Daniel 
Ndumbaro
Hakuna Chombo chochote cha TFF chenye mamlaka ya kumzuia au kumfungia Wakili wa kujitegemea kuwawakilisha wateja wake.
 
MALETA & NDUMBARO ADVOCATES inaandaa kesi ya madai dhidi ya TFF kwa kuizuia isifanye biashara yake halali.
MALETA
 & NDUMBARO ADVOCATES inapenda kuwajulisha wadau wote kuwa kupinga 
maamuzi ya Kamati ya Utendaji ya TFF sio kosa. Ikumbukwe kuwa JAMAL 
MALINZI aliwahi kupinga maamuzi ya FIFA, CAF na TFF kuhusu mabadiliko ya
 Katiba ya Mwaka 2013, kwa njia ya Circular Resolution, ili kuunda 
Kamati za Rufaa ya Uchaguzi, Kamati ya Maadili na Club Lincensing. 
Lakini leo Jamal Malinzi hataki kupingwa huyu ni dikteta.
 
 
Kwamba MALETA & NDUMBARO ADVOCATES inaandaa mashtaka dhidi ya Uongozi wa TFF, katika mambo yafuatayo:
Ubadhirifu wa US$ 200,000 fedha za TBL udhamini wa Taifa Stars
Kupinga Maamuzi ya FIFA kurejea Karume ( Haya yalikuwa mapendekezo haikuwa amri) Kufanya
 matumizi na manunuzi bila kibali cha kamati ya fedha ambayo ndiyo 
kamati ya manunuzi ya TFF kwa mujibu wa kanuni za manunuzi za TFF, 
manunuzi yaliyofanyika yanahusiana na Vifaa vya michezo wakati wa 
maboresho ya Taifa stars, Tiketi za ndege za Taifa Stars, timu ya 
wanawake na za vijana katika michezo yake na hotel za kambi ya timu ya 
Taifa ambapo hakukuwa na tenda zilizotangazwa wala ushindanishwaji wa 
aina yoyote jambo linaloashiria matumizi mabaya ya madaraka na fedha na 
kwa kuwa Rais ndiye msimamizi wa shughuli za sekretariet kikatiba jambo 
hili linakuwa pamoja na mengine ni suala la kimaadili kwa sheria za 
mpira.
 
Kwamba
 MALETA& NDUMBARO ADVOCATES inaandaa mashtaka dhidi ya Jamal Malinzi
 kwa Kupinga Maamuzi ya FIFA, CAF na TFF ili kufanya marekebisho ya 
Katiba mwaka 2013.
 
 
Tarehe
 21 Oktoba 2014, Dk. Damas Daniel Ndumbaro alikata rufaa dhidi ya uamuzi
 wa Kamati ya TFF lakini mpaka sasa Kamati ya Rufaa ya Nidhamu TFF 
haijasema lina inakaa. Tunatarajia kuwa haraka na dharura iliyotumika 
katika kuamua shauri katika kamati ya nidhamu itatumika pia kuamua 
shauri katika rufaa. Leo ni siku ya 10 toka rufaa ikatwe lakini bado 
kimya wakati ilichukua siku 2 tu kusikiliza kesi ya msingi.
 
KWAHIYO Dk. Damas Daniel Ndumbaro wa MALETA & NDUMBARO ADVOCATES kwa naiba ya wateja wetu tunasema kuwa:
Tutaendelea na kuwawakilisha wateja wetu kwa uadilifu wa hali ya juu. Kwamba madai yote tuliyoyasema katika barua ya awali dhidi ya TFF ikiwemo madai yanayohusiana na Mkutano Mkuu yapo pale pale.
 
 
Tumekata Rufaa dhidi ya maamuzi ya kamati ya nidhamu ya TFF kuanzia tarehe 21 Okotba 2014 Tunaandaa mashtaka dhidi ya Uongozi wa TFF kwa ubadhirifu wa fedha za umma Tunaandaa mashtaka dhidi ya TFF kwa kosa la kupinga agizo la FIFA kurejea Karume.
 
Tunaandaa
 Mashtaka dhidi ya Jamal Malinzi kwa kosa la kupinga Maamuzi ya TFF, CAF
 na FIFA katika mabadiliko ya Katiba ya TFF mwaka 2013.