Pages
▼
Friday, May 30, 2014
ZITTO KABWE ATOA UFAFANUZI JUU YA TUHUMA ZA KUOKOTEZA ZA SUGU
"Maelezo yangu kuhusu kazi za Kigoma AllStars/LEKADUTIGITE kwa NSSF na TANAPA.
Leo tarehe 29 Mei, 2014 Msemaji wa Kambi ya Upinzani kuhusu Habari,
Michezo, Vijana na Utamaduni amenituhumu kuhusika na kinachoitwa ufisadi
katika Shirika la TANAPA na NSSF.
Nasikitika kwamba katika hali
niliyonayo ya kumwuguza mama yangu naingizwa kwenye siasa za majitaka.
Kwa sasa nitatoa maelezo kwa ufupi ili kuondoa upotoshaji.
Kampuni ya LekaDutigite inamilikiwa na wasanii 15 ambapo kila mmoja ana
hisa 5% ambazo niliwalipia ili waweze kushirikiana katika kazi zao. Hisa
25% zilizobakia zinamilikiwa na kampuni ya Gombe Advisors ambayo ni
kampuni isiyofanya faida (Company limited by guarantee) na haina maslahi
yeyote ya kibiashara (not for profit company). Hivyo Mimi binafsi sina
maslahi yeyote ya kifedha zaidi ya kuwasaidia wasanii hawa katika kazi
zao mbalimbali.
Wasanii wa Kigoma AllStars wamefanya kazi na
TANAPA na NSSF, kazi ambazo zinajulikana na zipo. Kwa upande wa TANAPA
wasanii hawa waliandaa kazi ya kuitangaza Hifadhi ya Saadani na
walilipwa. Kwa upande wa NSSF wasanii hao walitunga wimbo na video yake (
http://m.youtube.com/watch?v=sMl8T-RkIdM ) na wimbo huo unatumika katika Shirika hilo.
Vile vile walifanya matamasha mbalimbali ya kuhamasisha watu kujiunga na NSSF. Wasanii wa Kigoma All Stars wote ni wanachama wa Mfuko huo.
Vile vile walifanya matamasha mbalimbali ya kuhamasisha watu kujiunga na NSSF. Wasanii wa Kigoma All Stars wote ni wanachama wa Mfuko huo.
Katika kazi zote hizi Mimi binafsi sijafaidika kwa namna yeyote ile
kifedha. Kauli yeyote ya kujaribu kuonyesha kazi hizi za wasanii ni
ufisadi ni kauli za kusikitisha na kukatisha tamaa kwa mtu ambaye
anajaribu kusaidia wasanii kufaidika na kazi zao za sanaa.
Toka
mwaka 2012 nilipoanza kujitokeza kusemea wasanii watu kadhaa wenye
maslahi na tasnia hii wamekuwa wakinikatisha tamaa na hata wengine kuona
nimewaingilia kazi zao.
Hivi sasa wasanii wa Kigoma AllStars ni wanahisa katika kampuni ya PERA Africa limited ili kufaidika na biashara ya miito ya simu. Yote haya nilifanya kwa uchungu nilionao kwa vijana wetu na sio kwa kutaka kufaidika kifedha. Nimeumizwa sana na tuhuma hizi za kuokoteza okoteza.
Hivi sasa wasanii wa Kigoma AllStars ni wanahisa katika kampuni ya PERA Africa limited ili kufaidika na biashara ya miito ya simu. Yote haya nilifanya kwa uchungu nilionao kwa vijana wetu na sio kwa kutaka kufaidika kifedha. Nimeumizwa sana na tuhuma hizi za kuokoteza okoteza.
Inaniumiza zaidi kutokana na ukweli kwamba
ninamwuguza mama yangu mzazi, kipindi ninachohitaji kutiwa moyo na
kuombewa hata na maadui zangu kisiasa. Kipindi ambacho mama yangu yupo
mahututi, tena mjumbe wa kamati kuu ya chama ambacho watoa tuhuma
wanatoka, pole ninayopewa ndio hiyo. Hakuna namna ya kukosa ubinaadamu
zaidi ya hivi.
Najua wajibu wangu ni kusimamia Mashirika ya Umma
na nikiwa mpigania uwajibikaji nipo makini sana kuhakikisha sina
mgongano wa maslahi katika mambo yangu. Ndio maana sina biashara yeyote
ile ili kuhakikisha natimiza wajibu wangu kwa uadilifu mkubwa. Napata
'moral authority' ya kutaka uwajibikaji kwa sababu nafanya kazi zangu
kwa misingi hiyo 'at arms length'.
Hivyo ninataka mara moja CAG
afanye ukaguzi wa kazi za wasanii hao kwenye NSSF na TANAPA. Pia
achunguze kama Gombe Advisors ( company limited by guarantee) ina
maslahi yeyote ya kifedha katika kazi hizo za wasanii. Nataka pia
Shirika la NSSF na TANAPA waweke wazi mchakato wa kazi zao na wasanii
hawa kupitia LEKADUTIGITE Limited.
Zitto Kabwe
Mei 29, 2014
Dar Es Salaam.
Mei 29, 2014
Dar Es Salaam.
MZUNGU AMLAZIMISHA MSICHANA KUFANYA MAPENZI NA MBWA JIJINI DAR

Mzungu huyo ambaye jina tunalihifadhi, alidaiwa kufanya
tukio hilo la kinyama Mei 26, mwaka huu na inadaiwa Aneth alipomkatalia,
alimtimua nyumbani hapo kwa kumtupia virago.
Chanzo makini kilidai kuwa, baada ya kutupiwa virago bila
kupewa mshahara wake sambamba na kipigo, Aneth aliripoti tukio hilo katika
Kituo Kidogo cha Polisi cha Tabata, Dar na muda mfupi polisi walifika nyumbani
hapo lakini Mzungu huyo hakutoka ndani, akakataa kuzungumza chochote
Taarifa zilidai kuwa, baada ya polisi kukutana na kizingiti
hicho, walimpigia simu kiongozi wao ambaye aliwaamuru warudi kituoni wajipange
upya.
Akisimulia zaidi ishu hiyo, Aneth alisema polisi
walipoondoka eneo hilo, umati uliochukizwa na kitendo hicho ulikusanyika nje ya
nyumba ili kumdhibiti ‘mtasha’ huyo kwa lolote.
Kuna jirani mmoja
alipiga simu tena kituo cha polisi alipoona hali ya hewa imechafuka ndipo
polisi wakafika kwa mara nyingine na difenda na kufanikiwa kuingia ndani kwa
kutumia geti kubwa, walipofika walikuta milango imefungwa lakini ilisemekana
aliruka ukuta na kutimkia kusikojulikana.
Polisi waliniambia
nimpigie simu ajisalimishe lakini nilipompigia alisema hayupo na kama
tunamhitaji tukutane sehemu huku na yeye akiwa na polisi wake
kilisema chanzo.

Mmiliki wa nyumba hiyo anayeishi Kigamboni, Mr. Cris alipoulizwa
kuhusiana na ishu hiyo, alikiri kupokea malalamiko na manyanyaso kutoka kwa
Aneth.
Akisimulia zaidi maisha anayoishi na Mzungu huyo, Aneth
alisema:
Alikuwa
akinitafutia sababu za kunitimua kwani hivi karibuni kwa bahati mbaya
nilipoteza ufunguo wa ndani, akanipiga mateke na kunisababishia maumivu makali
mwilini kiasi cha kushindwa kutembea.
Lakini lililoniuma
zaidi ni hili la kunilazimisha eti nifanye mapenzi na mbwa wake, amekuwa
akifanya hivyo mara kwa mara mimi nikaona siyo sawa na nilipokataa ndipo
yakanikuta hayo.
Aneth aliripoti matukio hayo katika Kituo Kidogo cha Polisi
Tabata na kupewa fomu ya matibabu (PF-3) sambamba na kufunguliwa jalada la kesi
namba TBT/RB/3132/2014/ SHAMBULIO na jalada la uchunguzi lenye namba
TBT/IR/1829/2014/UCHUNGUZI.