
 
Anaitwa
 Gabriel Munissi mkazi wa Mwanza ambae Polisi Ilala Dar es salaam 
ilithibitisha kwamba ndio amehusika kufanya mauaji ya watu wengine 
wawili kabla ya yeye kujiua huku ikiaminika ni kutokana na wivu wa 
kimapenzi.
Kama hukuipata hii taarifa ni kwamba:
Gabriel alikwenda Ilala na 
kusimama nje ya nyumba moja iliyokuwa na uzio na geti jeusi kusubiria 
atoke Mwanamke anaetajwa kuwahi kuwa mpenzi wake na kisha baada ya 
Mwanamke huyo kutoka huku akiendeshwa na mwanaume mmoja kwenye Toyota 
Surf na kukiwa na abiria wengine wawili kwenye gari. 
Gabriel ndio 
alianza kufyatua risasi hovyo, Shahidi alieshuhudia tukio hili mwanzo mwisho anasema waliamini 
kabisa kwamba Gabriel hakuwa jambazi kwa jinsi alivyoshambulia na 
kuendelea kubaki eneo la tukio bila kuwadhuru watu wengine waliokuwemo 
karibu, vilevile kama angekua jambazi isingekuwa rahisi kwa yeye kujiua.
Shuhuda anasema Gabriel alipiga risasi mpaka zilizokuwa ndani 
zikaisha ikabidi aongeze nyingine na kuendelea kushambulia huku akiwa 
hana nia ya kuwaua wale abiria wengine kwenye gari baada ya kuwajeruhi 
isipokua Mwanaume aliekua anaendesha pamoja na Mwanamke anaetajwa kuwa 
mpenzi wake ambae alikua amekaa pembeni ya dereva.
Hiki hapa chini ndio kitu cha mwisho alichokiandika Gabriel kwenye ukurasa wake wa facebook kabla ya kutenda unyama alioufanya.
Waliouwawa kwenye tukio hilo wanatajwa na polisi kuwa ni mwanaume aliekuwa anaendesha gari pamoja na mdogo wa Mwanamke anaetajwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Gabriel.
Baadhi ya marafiki wa Gabriel Mwanza wanasema Gabriel ni miongoni mwa vijana wa mjini waliokuwa wanaishi vizuri kwa kuendesha magari ya kifahari na kuwa na pesa za kutosha hivyo pesa haikuwa tatizo kwake.