Wachezaji
 waliozawadiwa kwa kungara katika michuano ya Airtel Rising stars  wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi  
Mkurugenzi wa maendeleo ya michezo nchini Leonard Thadeo (mwisho 
kulia) na katibu mkuu wa shirikisho la mpira wa miguu nchini Angetile 
Osiah(mwisho kushoto).
Mkurugenzi
 wa maendeleo wa michezo nchini bw Leonard Thadeo ameipongeza timu ya 
wasichana ya Tanzania baada ya kutwaa ubingwa wa vijana chini ya umri wa
 miaka 17 ya Airtel Rising Stars yaliomalizika juzi nchini Nigeria.
 
Tanzania
 waliibuka mabingwa baada ya kuwafunga Kenya katika fainali, pia 
amewapongeza wavulana baada ya kufikia hatua ya nusu fainali. Mabingwa 
wamezawadiwa kombe pamoja na kitita cha dola za marekani 10,000.
Katika
 pongezi zake pia amewapongeza wafungaji kwa upande wa wasichna ni 
Shelda Boniface na  mvulana  ni Athanas Mdamu na pia amempongeza 
mchezaji bora kutoka timu ya wasichana ambae ni Tatu Iddi .
 
Katika
 mashindano haya Tanzania imetoa rekodi tatu , mfungaji bora kwa upande 
wa wasichana  magoli matano, mfungaji bora wa kiume magoli manne , 
mchezaji bora kwa upande wa wasichana na pia wachezaji watatu upande wa 
wavulana wamefunga magoli matatu katika mechi moja (hat-trik) na 
kuondoka na mpira kila mmoja.
 
Kabla 
ya kukabidhiwa kombe na mabingwa hao , Mkurugenzi wa maendeleo ya 
michezo nchini bw Leonard Thadeo amesema kuwa serikali kupitia wizara ya
 michezo itaendelea kusaidi mpira wa vijana wenye umri mdogo ili 
kuifikisha mbali Tanzania katika medani ya soka.
 
Akiongea
 kwa niaba ya msafara wa timu kocha Rogacian Kaijage amesema kua 
mashindano yalikua magumu ila wamefanikiwa kuchukua ubingwa , 
amewapongeza vijana wake , kocha mwenzie wa timu ya wavulana Abel Mtweve
 na pia ameishukuru Serikali , Airtel , TFF, pamoja na  DRFA 
Kocha 
wa timu ya wasichana ya Airtel Rising stars Rogatician Kaijage akiongea 
wakati wa halfa ya kuwapongeza wachezaji wa timu ya Airtel Rising stars. 
Naodha
 wa timu ya wasicha ya Airtel Rising Stars chini ya umri wa miaka 17 
Stumai Abdalah akimkabidhi kombe la ubingwa Mkurugenzi wa maendeleo ya 
michezo nchini Leonard Thadeo. 
Kaptain
 ya timu ya wasichana Stumai Akikabidhi cheti cha kushinda kwa 
Mkurugenzi wa maendeleo ya michezo nchini Leonard Thadeo. 
Mchezaji
 wa timu ya wasichana Neema Paul pamoja na Mkurugenzi wa maendeleo ya 
michezo nchini Leonard Thadeo wakionyesha mfano wa hundi ya dolla 10,000
 iliyokabithiwa kwa timu ya washichana na Airtel baada ya kuibuka 
washindi wa michuano ya Airtel Rising stars Afrika. 
Chanzo: Michuzi 

