Inaripotiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Polisi katika wilaya ya Mufindi, PCD 
Ambwene Manyasi amewataka waganga wa jadi kuacha mara moja kuwapatia 
majambazi dawa za kutokukamatwa na polisi, na badala yake waganga hao 
wawapatie askari polisi dawa za kuwaona na kuwakamata wahalifu.
Eliasa
 Ally wa gazeti la Majira anaripoti kutoka Mufindi kuwa kauli na wito 
huo umetolewa na OCD huyo katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mufindi, 
wakati akizungumza na waganga wa jadi na tiba asilia kutoka Mudindi.
OCD
 amesema ni jukumu la kila mwananchi kuuchukia uhalifu na kulisaidia 
jeshi la polisi kutimiza wajibu wake. Amenukuliwa akisema ifuatavyo:
"Ninyi
 waganga wa jadi na tiba asili kazi yenu kubwa ni kutubu magonjwa 
yanayowasibu watu na siyo kutibu mbinu za majambazi ili wasiwe 
wanakamatwa wanapofanya uhalifu, hapo tutakuwa hatusaidiani, badala ya 
waganja kuwa wachonganishi, wawe waunganishaji wa wananchi, polisi na 
jamii. Badala ya kutoa dawa ya sisi polisi tusiwaone wala tusiwamamate 
majambazi, sasa nyinyi waganja mtoe dawa ya kutuwezesha kuwaona na 
kuwakamata kiurahisi majambazi wanaofanya uhalifu katika jamii yetu, huo
 ndiyo ushirikiano na polisi jamii tunayoizungumzia."
Aliwataka 
waganga hao kuhakikisha kuwa shughuli zao haziwi chanzo cha kutokea kwa 
maovu, kufumbia macho maovu na kusababisha jamii iwachukie waganga na 
polisi.
OCD alisema Jeshi la Polisi limejikita katika mambo 
makubwa matatu ambayo aliyataja kuwa ni polisi jamii, hali ya weledi na 
hali ya usasa.