Bwa. Mustafa Haji Abdinur 
mwandishi kutoka Somalia anayeandikia AFP akizungumza  mbele ya Baraza 
Kuu la  Usalama la Umoja wa Mataifa, wakati Baraza hilo siku ya Jumatano
 lilipojadili  usalama wa waandishi wa habari katika maeneo yenye 
migogoro,  Bw. Abdinur ambaye amejifundisha mwenyewe  uandishi  wa 
habari alieleza kwamba pale alipo ni kama maiti inayotembea na kwamba ni
 suala  la muda tu yeye kuuawa kutokana na ukweli kwamba waandishi 
wenzake wengi wamekwisha kuuawa nchini Somalia.  Hii ili kuwa ni mara ya
 kwanza kwa waandishi wa kimataifa kuzungumza ndani ya Baraza hilo.
 
 
 
  
Imeandikwa na Mwandishi Maalum, NY -- Baraza
 Kuu la Usalama  la Umoja wa Mataifa, jana jumatano liliendesha 
majadiliano ya wazi kuhusu usalama wa waandishi wa habari katika  maeneo
  yenye migogoro.
Majadiliano hayo yaliratibiwa na Marekani 
ambaye ni  Rais wa Baraza hilo kwa mwezi huu wa Julai, na kuhudhuriwa na
 waandishi wanne  wa kimataifa  ambao  walipata fursa ya  kuelezea 
masahibu wanayokumbana nayo  wakati wa kitekeleza majukumu yao.
Majadiliano
 kuhusu  suala la usalama wa waandishi wa habari katika maeneo yenye 
migogoro ni ya kwanza kufanyika ndani ya  Baraza hilo, tangu 
 lilipopitisha Azimio namba 1738 mwaka 2006 lililokuwa likizungumzia 
 suala hilo. Aidha hii pia ni mara ya kwanza kwa waandishi wa kimataifa 
kuzungumza ndani ya Baraza Kuu la Usalama.
“Hapa nilipo  mimi ni 
maiti anayetembea, ninatembea pasi kujua nani anaweza kuondoa uhai 
wangu,wakati wowote naweza kupotea maisha.  naweza kuuawa  hata na 
kijana mdogo ilimradi ana silaha”
Kauli hiyo ilikuwa ni ya Bw. 
Mustafa Haji Abdinur anayeandikisha  AFP akitoka Somalia. Na kuongeza 
kwamba rafiki zake wengi ambao ni waandishi wenziye tayari  wameshapotea
 maisha na kwamba kwa yeye
 
 
Bwa. Richard Engel kutoka NBC
 News mmoja kati ya waandishi wanne walioalikwa na Baraza Kuu la Umoja 
wa Mataifa  kueelezea uzoefu wao na  mikimikiki wanayokumbana nayo 
wanapotekeza majukumu yao ya kiuandishi.  Bw. Engel ambaye amesema 
amewahi kutekwa, alilitaka  Baraza Kuu la Usalama  linapojadilia kuhusu 
dhana nzima ya usalama wa waandishi, kujadili pia  ni nani hasa  
mwandishi wa habari  anaye stahili ulinzi na akahoji kama  wanaharakati 
ambao nao wanachukua picha  za matukio mbalimbali na kuzipost kwenye 
mablog kama nao ni waandishi wa habari.  pembeni yake ni Bi. Kathleen 
Carroll,  ambaye ni mhariri mtendaji wa  Associated Press na Makamu 
mwenyekiti wa Bodi ya Kamati ya  Kulinda   Waandishi ( CPJ) yeye  katika
 mchango wake alisema licha ya kwamba waandishi wengi wanapoteza maisha 
 wakati wakitafuta habari kwenye maeneo yenye migogoro lakini waandishi 
watano kati ya sita wanauawa  ndani ya nchi zao wakati wakitimiza 
majukumu yao.
  
 
  
kuwa hai mpaka sasa ni  kama bahati lakini ni suala la wakati tu.
Naye
  Bi. Cathleen Carrol  ambaye ni  Mhariri Mtendaji wa Associated Press 
na Makamu  Mwenyekiti wa Bodi ya Kamati ya    Kuwalinda Waandishi ( CPJ)
 pamoja na kuelezea  kwa uchungu mkubwa  matukio ya mauaji 
yaliyowakumbua waandishi wenzake katika  maeneo mbalimbali duniani 
 anasema, katika  shirika lao  kuna eneo ambalo  limetengwa maalum 
kwaajili ya kuwaenzi waandishi wote ambao wamepoteza maisha katika 
utekelezaji wa majukumu yao.
Kwa
 upande wake,  mwandishi Richard Engel wa NBC news, yeyé pamoja na 
kuelezea  mikasa mbalimbali ambayo amekwisha  kumbana nayo yakiwamo ya 
kutekwa wakati akiripoti matukio ya migogoro, yeyé alikwenda mbalia 
zaidi kwa kuuliza ni nani hasa mwandishi wa habari.
Bw,
 Engel alieza kwamba ulinzi wa waandishi wa habari hivi sasa unakuwa 
mgumu  sana tofauti na miaka  ya nyuma kutokana na kile alichosema 
kuibuka kwa makundi mengi yanayofanya kazi za  waadishi wa habari.
“
 Wakati tukijadili  hoja hii ya  usalama wa waandishi wa habari, pengine
 pia ni muhimu tukajiuliza hivi ni nani hasa mwandishi wa  habari,  je 
mwanaharakati anaye shika  video au kamera na  kalamu je naye ni 
mwandishi,  au je na yule  mwanamgambo mwenye silaha lakini naye 
ameshika  kamera na kupiga picha  je naye   ni mwandishi” akahoji Bw, 
Engel 
Anasema kwamba
 ni jambo la kawaida hivi  unapokwenda kwenye tukio fulani  kukutana na 
makundi ya watu kila mmoja akiwa ameshika kamera yake akichukua matukio,
 na katika mazingira kama haya,  ni vigumu kwa vyombo vya ulinzi na 
 usalama kutofautisha nani hasa ni mwadishi aliyesomea na kubobea kwenye
 fani hiyo na yupi  mwanarakati. 
Kwa
 maoni yake anasema  pamoja  na hamu ya kila mtu kutaka kutaka 
kukukusanya habari na kuzisambaza kupitia mitandao ya kijamii,  ni vime 
kujiuliza  nani anastahili na anapwashwa kupewa ulinzi anapotimiza 
majukumu yake na kwa vyovyote vile anasema kama ilivyo kwa 
wanadiplomasia ambao wanakinga vilevile waandishi waliosomea na wenye 
weledi na taaluma yao wanatakiwa kupewa ulinzi.
Majadiliano
 hayo yalifunguliwa na  Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. Jan 
Eliasson,  na yalikuwa na mvuto wa ina yake  hasa kutoka na kauli 
zilizokuwa zikitolewa na baadhi ya wachangiaji.
Kwa
 upande wake  Naibu Katibu  Mkuu alieleza kwamba  hujuma dhidi ya 
waandishi wa habari ni jambo lisilokubalika kwa kile alichosema ni 
kubinya  uhuru wa  upatikanaji na utoaji wa habari, lakini pia ni 
ukiukwaji wa uhuru wa kujieleza. Akalipongeza  Baraza kwa kuitisha 
mjadala huo
Akasema 
 karne iliyopita waandishi wa habari wapatao 600 walipoteza maisha 
katika matukio mbalimbali  na wengine wakiishia magerezani, huku 
asilimia 90 ya matukio hayo hakuna hatua zozote za kisheria 
zilizochukuliwa.
Pamoja
 na wachangiaji wengi kukiri kwamba  mazingira ya  ufanyaji kazi kwa 
waandishi wa  habari yamezidi kuwa magumu na hatari,  walielezea pia 
 kwamba mazingira hatarishi  hayapo tu katika maeneo yenye vita bali 
 hata katika nchi wazofanyia kazi. Ambapo takwimu kutoka  CPJ 
zinaonyesha  katika kila waandishi  watano kati ya sita wanauliwa wakiwa
 ndani ya nchi zao.
Wengi
 wa wazungumzaji walieleza kwamba  baadhi ya waandishi ama wamekuwa 
wakitishiwa maisha yao na familia zao au hata kupoteza maisha  kwa 
kuandika  na kuchapicha habari zinazofichua  vitendo vya rushwa , 
vitendo vya jinai au kashfa zinazohusu makundi mbalimbali ya jamii na 
 vilevile kuandika habari za uchochezi  kati ya  kundi moja na jingine..
Wengine
 wakaenda mbali kwa kusema  wakati mwingine waandishi wenyewe wanajiweka
 katika mazingira ya hatari kwa kukiuka misingi ya kazi zao, kwa 
kuandika habari zinazopendelea  upande mmoja, au kufanya kazi kinyume 
cha  matakwa na matarajio ya yule anayemfanyia kazi. 
Wazungumzaji
 hao wakatoa wito kwa  Baraza kuu la Usalama kuangalia namna  bora ya 
kuboresha ulinzi wa waandishi wa habari katika mazingira  hatarishi kama
 vile vita na migogoro na pia wakatoa wito wito  kwa waandishi wa habari
 kuzingatia  misingi ya taaluma zao na kuepuka kujingiza katika mitengo 
isiyo  ya lazima.
Suala
 lingine lililozungumwa kwa  kina ni lile la kutofikishwa mbele ya mkono
 wa sheria watu wanaotuhumiwa  kuwahujumu waandishi wa habari.