Akizungumza na gazeti la NIPASHE lililochapisha habari ya dawa za 
kulevya kilo 150 zilizokamatwa kwa wasichana wa Kitanzania nchini Afrika
 Kusini, Kamanda wa Polisi Kikosi cha Viwanja wa Ndege Nchini, Deusdedit
 Kato, amesema tukio hilo ni baya, limeifedhehesha Tanzania na kuiitia 
dosari nchi ambayo ilisifika kuwa na watu waminifu.
Hivyo amesema kuna haja ya kusaidiana ili kurudisha imani kwa nchi.
“Ni
 lazima tupambane kurudisha heshima kwa sababu watanzania watakuwa 
hawaaminiki tena katika nchi nyingine, ni  mapema mno kuinyoshea kidole 
taasisi yeyote kwani uchunguzi bado unaendelea ili kubaini aliyeruhusu 
kupitisha mzigo huo, ”alisema alipoulizwa na gazeti hili kama wasichana 
hao walikaguliwa.
Alisema ni lazima kwa pamoja kufanya uchunguzi 
na kubaini ni taasisi gani ilipwaya katika kutekeleza majukumu yake 
ipasavyo na kuruhusu dawa hizo kupita.
Alisema mpaka sasa uchunguzi umefikia katika hatua nzuri na watatoa taarifa wakati wowote.
Alizitaja Taasisi hizo kuwa ni Polisi,Usalama wa Taifa,Uhamiaji na Mamlaka ya Viwanja vya ndege (TAA).
“Tukio
 hili ni baya limeiitia dosari nchi ambayo ilisifika kuwa na watu 
waminifu lakini sasa limetuchafua sana, tunahitaji kusaidiana ili 
kurudisha imani kwa nchi yetu iliyokuwapi hapo awaliaaaa,” alisema na 
kuongeza: "Wasichana hao inadaiwa kuwa walisafirisha dawa hizo kwa ndege
 ya Shirika la Ndege la South African Airways linalomilikiwa na serikali
 ya Afrika Kusini."
Hadi sasa wasichana hao bado wanashikiliwa na   Jeshi la Polisi la Afrika Kusini kwa ajili ya upelelezi.