  | 
| Picha onayoonesha mchoro wa jengo | 
Na: Belinda Kweka- MAELEZO
CHUO
 Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili(MUHAS)  kipo katika mpango wa 
kujenga chuo kipya kwa ajili ya ufanyaji mazoezi kwa wanafunzi.Ujenzi 
huo  unatarajiwa kuanza Agosti mwaka huu katika eneo la Mloganzila 
Kibamba  ambapo , ukimalizika  utachukua wanafunzi 15,000  watakaosoma  
taaluma  mbalimbali za afya. Akizungumza  na
waandishi wa habari  leo
 kwenye   Maonesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa  yanayoendelea katika 
viwanja  vya  Mwalimu  J. K Nyerere  jijini  Dares Salaam (sabasaba) 
,Afisa Mipango Mkuu wa chuo hicho Ulimbaga Kijobile alisema  uamuzi  huo
 umetokana na ongezeko la wanafunzi ni wengi.
Alisema  eneo hilo   
lita wezesha wanafunzi hao kupata sehemu  za kusomea kwa ufanisi  kama 
vile  ya maabara za kisasa, madarasa, na sehemu za ufanyaji mazoezi.
“Tumeamua
 kuanzisha mradi kwa kujenga chuo kipya kwa sababu MUHAS ina sehemu 
ndogo na hatuwezi kuipanua kwa ajili ya kuongeza ukubwa wa chuo ili 
kuweza kutosha kwa wanafunzi” alisema Kajobile.
Aidha alisema 
wanafunzi hao , walikuwa wakipata tabu katika kufanya mazoezi ,hivyo 
hulazimika  kwenda  hospitali za Mwananyamala na Amana.“Muda mwingine 
tunatumia hospitali nyingine ili kupata sehemu ya kutosha lakini 
hospitali hii itakayojengwa itasaidia kuchukua wanafunzi wote ili kuweza
 kufanya mazoezi yao bila usumbufu” alisisitiza Ulimbaga.
Alisema  
ujenzi wa  chuo hicho, kinakadiriwa kujengwa ndani ya mwaka 
mmoja,ambapo  wanafunzi wa muhula wa kwanza wa mwaka 2015 wanatarajiwa 
kuanza.
Aliongeza  kuwa kitatoa huduma za kiafya kama hospitali 
nyingine hivyo wananchi wa eneo hilo wanashauriwa kufika mara baada ya 
ufunguzi wa chuo hicho ili kupata matibabu mbalimbali.