TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Marekani, Mhe. Barack Obama anatarajiwa kuwasili nchini tarehe 01 Julai, 2013 mchana kwa ziara ya kitaifa ya siku mbili.
Katika
 Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam, 
Mhe. Rais Obama ambaye atafuatana na Mkewe Mama Michelle atapokelewa na 
Mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya 
Mrisho Kikwete.
Baada ya mapokezi, Mhe. Rais Obama atakwenda 
Ikulu kwa mazungumzo rasmi na Rais Mhe. Kikwete. Aidha, atafanya mkutano
 na Wafanyabiashara na kuhudhuria Dhifa ya Kitaifa.
Tarehe 2 
Julai 2013, Mhe. Rais Obama atatembelea Mitambo ya kufua Umeme ya 
Symbion iliyopo Ubungo, Dar es Salaam na kuzindua rasmi Mpango Maalum wa
 Maendeleo ya Nishati Barani Afrika ulioanzishwa na  
  
Marekani (Power Africa Initiative).
Mpango huo utaanza na nchi saba ambazo ni: - Tanzania, Kenya, Uganda, Ethiopia, Ghana, Nigeria na Sudan Kusini.
Mhe. Rais Obama anatarajiwa kuondoka nchini tarehe 02 Julai 2013.
IMETOLEWA NA:
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA,
DAR ES SALAAM
30 JUNI, 2013
 
 
Monday, July 1, 2013
- On Monday afternoon, President Obama takes part in a formal arrival ceremony in Dar es Salaam, Tanzania.
 
- President Obama participates in a bilateral meeting and joint press conference with President Jakaya Kikwete of Tanzania.
 
- In the evening, President Obama participates in a CEO roundtable and business leaders forum.
 
- President Obama and President Jakaya Kikwete of Tanzania participate in an official dinner.
 
Tuesday, July 2, 2013
- On Tuesday morning, President Obama takes place in a Consulate meet and greet.
 
- President Obama visits the Ubungo Power Plant.
 
 
 
 
Atakapowasili
 katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere na ndege yake  
Air Force One, Rais w Maekani, Barack Obama atazindua barabara mpya 
upande wa Mashariki wa lango la kuingia Ikulu ambayo inatarajiwa kuitwa 
Barack Obama.
Baada ya shughuli hiyo atazungumza kwa nyakati 
tofauti na wafanyabiashara wa nchi za Afrika na Marekani kwenye hoteli 
ya Hyatt Regency,  Dar es Salaam.  Amepanga pia kuzungumza na maofisa wa
 Ubalozi wa Marekani nchini.
Baadaye atahudhuria dhifa ya taifa usiku ambayo imeandaliwa na mwenyeji wake Rais Jakaya Kikwete, Ikulu, Dar es Salaam.
Kesho
 ataweka shada la maua sehemu ulipokuwa Ubalozi wa Marekani ikiwa ni 
kumbukumbu ya watu waliouawa katika shambulizi la kigaidi la bomu mwaka 
1998, Dar es Salaam. Pia atatembelea mitambo ya kufua umeme ya kampuni 
ya Symbion iliyoko Ubungo.
Rais Obama atatoa hotuba kuzungumzia mikakati ya Marekani ya kusaidia Afrika kuzalisha nishati ya umeme.
Michelle
 atakuwa na ratiba yake ambapo atapata staftahi na mwenyeji wake, Salma 
Kikwete katika ofisi za Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (Wama), Dar es 
Salaam.
Pia atatembelea sehemu ulikokuwa ubalozi wa Marekani na 
kisha atashuhudia onesho la utamaduni la kikundi cha Baba wa Watoto, 
ambacho kinajumuisha watoto wa mitaani wenye umri wa kuanzia miaka 
mitano hadi 18 kwenye Makumbusho ya Taifa.
Jumanne, Michelle 
atahudhuria mkutano na wake wa marais wa nchi za Afrika ambao pia 
utahudhuriwa na mke wa Rais wa zamani wa Marekani, George Bush, Laura.
Julai
 2, Rais Obama atatembelea mitambo ya kufua umeme ya Symbion Ubungo saa 4
 asubuhi na kisha msafara wake utapita Nelson Mandela, Tazara hadi 
uwanja wa ndege na kuondoka saa 5.20 asubuhi.
Obama ametangaza 
mpango wa kuwajengea uwezo viongozi vijana wa Afrika kwa kuwapa mafunzo 
ya uongozi katika vyuo vikuu vya Marekani hasa katika masuala ya 
utawala, biashara na uongozi.
Katika hotuba yake katika Chuo 
Kikuu cha Johannesburg juzi jioni, alisema hatma ya Afrika iko mikononi 
mwa vijana; hivyo ni lazima wawezeshwe ili kuliongoza vizuri bara hili.
Alisema
 mafunzo hayo yatatolewa  chini ya mpango wa ufadhili wa Marekani kwa 
viongozi vijana ambao utawajengea uwezo wa kuendesha huduma za 
kiserikali ikiwa ni pamoja na biashara na   kuhudumia jamii yao.
Kuanzia
 mwaka ujao Marekani itatoa mafunzo kwa vijana 500 ambayo yatakuwa ya 
wiki sita ambapo idadi hiyo itaongezeka hadi vijana 1,000 kila mwaka.
Watakaofadika
 ni vijana wa kati ya umri wa miaka 25 hadi 35 ambao wamekuwa 
wakijihusisha na uongozi  ndani ya Serikali, sekta binafsi na asasi za 
kiraia. Alisema washiriki hao ni lazima waoneshe dhamira yao katika 
kuitumikia jamii.
Obama alisema Afrika ina mwonekano mzuri kwa 
siku zijazo na kuwataka vijana wa Afrika kuhakikisha wanatumia uwezo wao
 katika kutumikia bara lao.
Mpango wa kuendeleza vijana wa Afrika
 ujulikanao kama YALI ulizinduliwa mwaka 2010 na Rais Obama ikiwa ni 
sehemu ya kusaidia maendeleo, kuhamasisha ujasiriamali na kujenga uwezo 
wa Afrika kuwa na viongozi bora wa kizazi kijacho.